Digg StumbleUpon LinkedIn YouTube Flickr Facebook Twitter RSS Reset

5 DHAHABU na feza haziniokoi

image_pdfsauvegarder en PDF-Saveimage_printImprimer-Print

1. Dhahabu na fedha haziniokoi, Hazina na mali haziponyi roho,
Lakini kwa damu ya Yesu mwokozi nimenunuliwa nipate uhuru.

Refrain :
Nimekombozwa pasipo mali, kwa neema nimeokoka !
Ni bei ghali : kwa damu yake Alilipa deni langu.

 

2. Dhahabu na fedha hazinilipii madeni makubwa ninayo kwa Mungu.
Mwokozi alinikomboa kwa damu nipate wokovu, nitoke dhambini

 

3. Dhahabu na fedha haziufungui Mlango wa ku’karibia mwenyezi,
Lakini kwa damu nimeifikia Neema ya Mungu aliya mkuu.

 

4. Dhahabu na fedha hazinifikishi nyumbani mwa Mungu niliyemwasia,
Lakini nimekombolewa kwa damu, kwa hiyo nitachukuliwa mbinguni.


 

 

No comments yet.

Leave a Comment