Digg StumbleUpon LinkedIn YouTube Flickr Facebook Twitter RSS Reset

49 NJIA yote naongozwa kwa mkono wa Mwokozi

image_pdfsauvegarder en PDF-Saveimage_printImprimer-Print

 49

1. Njia yote naongozwa kwa mkono wa Mwokozi, ninapo wema wake, sina shaka, hofu tena. Nina raha ya mbinguni, ninakaa kwa salama. :/: Na katika mambo yote ananitendea mema. :/:

2. Njia yote naongozwa, namtegemea Yesu. Anilinda jaribuni, anitia nguvu pia. Nikiona kiu hapa, nikichoka safarini,:/: Mwamba uliopoasuka unabubujika maji. :/:

3. Njia yote naongozwa kwa mkono wake bora, atanituliza tena kwa babake huko juu. Miguuni pake Yesu ninataka kusujudu,:/: Nakusifu yeye, kwani aliniongoza huku. :/:

Fanny Crosby, R. Lowry, 1875
All the way my Saviour leads me, R.S. 445

No comments yet.

Leave a Comment