14 MWOKOZI wangu ulikwenda juu kukaa kuumeni kwake Baba

1. MWOKOZI wangu ulikwenda juu kuumeni kwake Baba;

Utakusanya sisi sote huko, Mbinguni kwako utatufikisha.

:/: Makao mema wa’tulinda, Unatungoja kwake Mungu Baba. :/:

 

2. Mwokozi wetu wewe, Yesu Kristo, kwa’ajili yetu mbele yake Baba.

Wachungu sana sisi, kundi lako, Na watusaidia ‘jaribuni.

:/: Na sikuzote unatuombea, watushindia vita kaili huku. :/:

 

3. Mikono yako uliwanyoshea walio wako, siku uli’kwenda;

Na hivyo siku utakaporudi utabariki wakuaminio.

:/: Ulivyokwenda, utakavyorudi; Niombe, nikakeshe kwa imani!:/:




55 TUPATE kwa nani faraja ya roho




73 NAJUA njia moja ya ku’fikia mbingu

73

1.Najua njia moja yakufika mbinguni, ingawa ikipita katika majaribu, lakini iendako mjini huko juu, :/: Na njia hiyo Yesu. :/:

 

2.Najua na amani iliyo ya milele, huwezi kuipewa kwa fedha na dhahabu; ni tunu ya rehema iliyotoka Baba. :/: Amani hiyo Yesu. :/:

 

3.Najua nguvu moja yakuniponya roho, initiayo raha, amani na faraja, inanilinda vema na nguo yangu safi, :/: Na nguvu hiyo Yesu:/:

 

4.Najua na kifiko mbinguni huko juu, na siku ni karibu kita’poonekana. Yafa’kukaza mwendo, kupiga mbio sana! :/: Kifiko ni mbinguni. :/:

Hildur Elmers, 1894




88 MPONYI apitaye wote amefika hapa

88

1. Mponyi apitaye wote amefika hapa. Awaponyesha watu moyo. Yesu wa upendo.

Pambio:
Jina linalopita yote juu na chini pote pia, jina kubwa, jina jema: Yesu wa upendo.

 

2. Awasamehe watu dhambi wakizitubia, awapokea kwa neema, waipate afya.

 

3. Tukiwa na masikitiko, Yesu afariji. Akitubarikia sana, woga waondoka.

 

4. Watoto walipenda sana jina lake Yesu, liwalindalo na mabaya, wakijaribiwa.

 

5. Shetani aogopa sana jina lake Yesu. Katika vita ju’ ya dhambi latutia nguvu.

 

6. Mbinguni tena kwa furaha tutamwona Yesu. Tutasahau shida zote, tutamshukuru.




89 NAJUA jina moja zuri

 89

1. Najua jina moja zuri, lapita kila jina huku, lanipa raha na amani, na jina hilo Yesu.

Pambio:
Yesu, jina zuri mno! Yesu, unapenda wote, Yesu, tunalindwa vema katika jina lako.

 

2.Napenda jina hilo jema, linanivuta kwake Mungu. Na katika huzuni yangu lanifariji sana.

 

3. Siwezi mimi kueleza uzuri wake jina hili, lakini namwimbia Yesu, nasifu jina lake.

W.C. Martin, 1901
The name of Jesus is so seet, R.S. 4




90 YESU Yesu jina kubwa

90

1. Yesu, Yesu, jina kubwa, nyimbo zao malaika! :/: Limekuwa ndani yangu mto wa furaha bora:/:

 

2.Jina lake kama nyota, linanionyesha njia. :/: Katika jaribu, shida, na usiku duniani. :/:

 

3.Ni mikono ya upendo yenye kunikumbatia. :/: Hapo najificha vema, kama chombo bandarini.:/:

 

4.Jina hilo liwe kwangu, wimbo wa safari yangu! :/: Niletewe wema nalo, toka nchi nzuri juu! :/:

Carl Boberg
Jesus, Jesus, o, Det, Sgt. 256




91 YESU jina ili njema lichukuwe siku zote!

 91

1. Yesu, jina hili jema, lichukue siku zote! Lina raha na faraja, lichukue uendako!

Pambio:
Jina kubwa, jina zuri la matumaini yetu! Jina kubwa, jina zuri la furaha ya mbinguni!

 

2. Lichukue jina hilo, lenye nguvu yakushinda! Ukijaribiwa huku, taja jina lake Yesu!

 

3. Yesu, jina jema mno, latutia shangwe kubwa, ni makimbilio yetu, ngome, msaada pia.

 

4. Na kwa jina lake Yesu kila goti litapigwa, watu wote watakiri kwamba Yesu ni Mfalme.

 

Take the name of Jusus with you, R.S. 465

[youtube https://www.youtube.com/watch?v=TRj3urquuZU?feature=oembed&w=500&h=281]




92 YESU! jina ili ninapita kila jina duniani pote

92

1. Yesu! Jina hili linapita kila jina duniani pote. Yesu, Yesu! Jina hilo ni marhamu iliyomiminwa.

Pambio:
Jina hili ni lenye nguvu ya kuondoa dhambi zangu zote. Yesu, Yesu! Jina hilo lanitia shangwe na furaha.

 

2. Si jingine jina duniani lenye nguvu, kweli na uzima. Yesu, Yesu! Jina hilo waliloimbia malaika.

 

3. Jina hili lina wema mno, limejaza mbingu tangu mwanzo. Yesu, Yesu! Jina hilo, litaimbwa duniani pote.

 

4. Sitaweza kusahahu Yesu, jina lake ni wokovu wangu. Yesu, Yesu! Nitamwona huko kwake tena kwa furaha.




102 SAYUNI ulaki Bwanako




118 NI MWOKOZI mzuri ninaye

118

1. Ni Mwokozi mzuri ninaye, alikufa kunikomboa. Alitoa uzima wake kwa ajili ya watu wote.

Pambio:
Alikufa msalabani, alikufa msalabani. Kwa ajili ya dhambi zangu zote alikufa msalabani.

 

2. Aliacha makao juu, akafika ulimwenguni; aliteswa kwa’jili yangu na kunifungulia mbingu.

 

3.Dhambi zangu ali’chukua, kujitwika hukumu yangu, na alijeruhiwa ili aniponye na ‘nipa raha.

 

4. Bwana Yesu alifufuka, akarudi mbinguni kwake; na yuaja upesi tena achukue walio wake.

 

F.A. Graves




120 MSALABANI nilimuona Yesu

120

1. Msalabani nilimwona Yesu, Mwokozi wangu aliyeniponya; rohoni mwangu giza ikatoka, ninafuata Yesu sasa.

Pambio:
Nimeokoka kutoka dhambi, na siku zote ninaimba kwa furaha. Ni vita kali kushinda yote, lakini Yesu yu karibu.

 

2. Mwokozi wangu ananipa nguvu, nikiuona udhaifu huku. Na vita yote itakapokwisha, nitaipata raha kwake.

 

3. Mwokozi wangu, ninakufuata, furaha yako inanituliza. Na siku moja utakuja tena kunichukua huko kwako.




121 YESU nifuraha yangu

121

1. Yesu ni furaha yangu, amejaa pendo kweli. Anaweza kusimika kila mwenye udhaifu. Ananipa ujasiri, nguvu, raha na faraja. Hata nikionja kufa, Yesu ni mchunga wangu.

 

2. Nimefungwa na Mwokozi kwa kifungu cha upendo, hata kufa hakuwezi kunitenga naye Yesu. Mimi wake siku zote, ninataka kumtii. Kwa neema nimepona, nisitumikie dhambi.

 

3. Kwa mikono ya upendo ninakumbatiwa naye, sitaweza kutafsiri pendo lake kubwa kwangu. Napokea nguvu yake, yanijaza moyo wangu. Yesu ananiongoza katika safari yangu.

 

Torvald Löwe

[youtube https://www.youtube.com/watch?v=PLUzSsPGjs4?feature=oembed&w=500&h=281]

 

 

[youtube https://www.youtube.com/watch?v=l2rxXFUp0Tk?feature=oembed&w=500&h=281]




122 MWOKOZI kamili ni Yesu pekee

122

1. Mwokozi kamili ni Yesu pekee, Mwokozi mzuri halisi. Katika wokovu wa Mungu mkuu ninalindwa naye kabisa.

Pambio
Katika wokovu nalindwa salama, naishi kwa maji ya ‘hai. Upendo wa Mungu unanizunguuka :/: na kanihifadhi daima. :/:

 

2. Baraka ya mbingu inanijaliza kwa Roho ya utakatifu. Nasifu Mwokozi katika furaha, wokovu umenifikia.

 

3. Mwokozi mzuri ni Yesu pekee, aniondoaye mizigo. Njiani ananiongoza vizuri, anipa na nguvu ya mwendo.

 

4. Nitakapomwona Mwokozi mbinguni baada ya shida za huku, Nitamhimidi na kumshukuru Bwana ninayempenda.

Fanny J. Crosby, 1903




123 MWOKOZI mzuri ninaye

123

1. Mwokozi mzuri ninaye, zamani sikumfahamu, na sasa ninamhubiri, wengine wapate kuona.

Pambio:
Wote watamwona, wote watamwona Mwokozi mzuri ninaye; Lo! Wote watamwona.

 

2. Shetani akinizuia nisimfuate Mwokozi, najua Bwanangu hodari hutaka kunisaidia.

 

3. Apita wo wote kwa wema, mfano ‘tukufu wa Baba, lakini anitaja ndugu, niliye maskini kabisa.

 

4.Natoa maisha na pendo kwa Yesu aliyenipenda. Katika ishara za Mungu upendo wapita yo yote.

Carrie E. Breek, 1902
I have such a wonderful Saviour, R.H. 640




128 NINA rafiki mwema

 128

1. Nina rafiki mwema, naye alinifilia; alinivuta kwake na amenifanya mpya. Ni mali yake Yesu tu, ninaongozwa naye, alikomboa mimi kwa agano la upendo.

 

2.Nina rafiki mwema, na aliondoa dhambi, aliniweka huru na kunipa Roho yake. Na vitu vyote ninavyo ninavitoa kwake, maisha yangu ni yake, yaimba sifa zake.

 

3.Nina rafiki mwema na anayeweza yote, pamoja naye Yesu tu nashinda majaribu, atanitwaa kwake ju’ mbinguni kwa furaha; Nitastarehe katika makao ya milele.

 

J.G. Small
I have a friend,




132 YESU mwokozi unanipenda

1. Yesu Mwokozi, unanipenda, na pendo lako ni kubwa kabisa. Ulinivuta karibu nawa, Mimi ni wako daima dawamu.

 

2. Yesu Mwokozi, unanipenda, na pendo lako lapita akili. Linanifunza kuzifahamu raha, upole na utu adili.

 

3. Yesu Mwokozi, unanipenda, mimi maskini, dhaifu, mnyonge. Nimetakaswa kwa damu yako; ninakuomba, ‘nijaze upendo!

 

4. Yesu Mwokozi, unanipenda, umenitilia wimbo kinywani wa kukusifu hata milele, nitakuona halisi mbinguni.




167 NINAJUA Rafiki mwema

 167

1. Ninajua rafiki mwema, anitunza sana kila siku. Ayaponya majeraha na machozi ayafuta. Jina lake ni Yesu Kristo.

Pambio:
Najua rafiki mwema, na yeye ajaa ne’ma. Nikiomba asikia, afariji nikilia. Ndiye Yesu, na si mwingine.

 

2. Nimepata rafiki mwema, afariji na kunipa raha. Nikitegemea yeye sitahofu maadui; na rafiki ni Yesu Kristo.

 

3. Nifikapo mtoni pale paitwapo “kufa” na “mtego”, sitafadhaika hapo, Yesu atakuwa nami; ni rafiki mkubwa mno.

 

4. Pwani nzuri ya huko juu nifikapo kwa neema kuu, nitaimba kwa kinubi, nitasifu Yesu sana kwa upendo na urafiki.

Peter Blhorn, N. Cronsie, 1914
Oh, the best friend to have is Jesus, R.S. 88




177 NIPE habari ya Yesu

177

1. Nipe habari ya Yesu, uiandike rohoni! Uniimbie zaburi ya kumsifu Mwokozi, sifa iliyotangazwa na malaika zamani: Mungu wa ju’ atukuzwe, iwe amani duniani!

Pambio:
Nipe habari ya Yesu, uiandike rohoni! Uniimbie zaburi ya kumsifu Mwokozi!

 

2. Nipe habari ya Yesu, jinsi alivyohimili shida, jaribu na teso na umaskini na bezo (sic)! Maradhi zangu (sic) na dhambi aka’chukuwa mwenyewe, kila wakati tayari kusaidia wahitaji.

 

3. Nipe habari ya Yesu, ya msalaba na kufa, taja kaburi mwambani, alipotoka Mwokozi! Pendo la Yesu ni kubwa, aliyekufa Golgotha, akafufuka hakika, namshukuru siku zote!

Frances J. Crosby-van Alstyne
Tell me the story of Jesus, R.S. 456; R.H. 150; MA. 206




192 SAUTI moja iliniuliza

192

1. Sauti moja iliniuliza: ” Wajua nilikufanyia nini? :/: Kwa’jili yako niliteswa sana; ufike kwangu, kwani nakupenda! ” :/:

 

2. ” Nilipokuwa huku duniani wakanitia taji ya miiba, :/: Na sikupambwa fedha na dhahabu, lakini majeraha na uchungu.” :/:

 

3. ” Golgotha nilifika siku moja, na nilikufa ju’ ya msalaba. :/: Tazama, katika mikono yangu nimekuchora, e’ mtoto wangu.”:/:

 

4.Heleluya, rohoni ninaimba! Nimejiweka mikononi mwake. :/: Na Yesu ananiongoza sasa, nifike nchi nzuri huko juu. :/:

K.E. Svedlung




219 HATUMUJUI rafiki mwema

 219

1. Hatumjui rafiki mwema, ila Yesu, ila Yesu; yeye mwenyewe atufahamu, yeye Bwana peke yake.

Pambio:
Yesu anatujua, pia Yesu anatuonya njia. Yesu rafiki kupita wote, wote, wote pia wa dunia.

 

2. Hatumjui rafiki mwema kama Yesu, Bwana Yesu. Na pendo lake ni la ajabu, linadumu siku zote.

 

3. Je, ataweza kutusahau? Hataweza ku’sahau. Twafarijiwa kwa pendo lake kila siku, kila siku.

 

4. Nani ashika agano lake? Bwana Yesu peke yake. Alikataa kusaidia? Hataweza kukataa.

 

5. Nani rafiki mpendwa wangu? Bwana Yesu peke yake. Anastahili kupata sifa huku chini na mbinguni.

Johnson-Oatman
There’s not a friend, RH. 110




240 NAVUTWA kwake Yesu na ninamufurahiya

240

1. Navutwa kwake Yesu na ninamfurahia, uzuri wake unapita vyote vya dunia. Siwezi kuupima kweli kwa fikara zangu. Uzuri wake unazidi kuwa bora kwangu!

Siwezi kueleza uzuri wake huku, lakini niaufahamu huko ju’ mbinguni.

 

2. Upendo wa ajabu mno nausifu sana, ukanivuta kwa upole, nije kwa Bwana! Ukaondoa mimi katika unyonge wangu, upendo wake unazidi kuwa bora kwangu!

Siwezi kueleza uzuri wake huku, lakini nitaufahamu huko ju’ mbinguni

 

3. Wokovu wake wakupendwa mno nausifu, uliondoa woga, ukanipa utulivu. Napenda Yesu aliyechukuwa dhambi zangu, wokovu wake unazidi kuwa bora kwangu.

Siwezi kueleza wokovu wake huku, lakini nitaufahamu huko ju’ mbinguni.

W.C. Martin




280. JINA lake Yesu linadumu

280

1. Jina lake Yesu Kristo linadumu siku zote; jina hili la milele haliwezi kunyauka; linafaa watu wote, na wazee na vijana; linaweza kuongoza kila mtu kwake Mungu.

Pambio:
Jina hili nalipenda, limewasha moyo wangu; na kwa jina hili jema nimepata kuokoka.

 

2. Jina hili linavuma pande zote za dunia, na kwa wote linaleta tumaini na faraja. Jina hili laondoa uadui na ubaya, hata milki ya Mwokozi itaanza kutawala.

 

3. Na katika giza huku jina hili linang’aa, laonyesha msafiri njia wazi ya uzima. Jua likitiwa giza, jina hili linadumu; na milele lisifiwe hapa na mbinguni juu.




283. NIMEYASIKIA mengi aliyoyafanya Yesu

283
1. Nimeyasikia mengi aliyoyafanya Yesu katika maisha yake huku chini: Pote alitenda mema, alisaidia wote. Kwa furaha ninaimba: “Yesu yeye yule leo!”

Pambio
Yesu Kristo yeye yule jana, leo, siku zote. Hutafuta wapotevu, huokoa na waovu. Mwokozi wetu yeye yule!

 

2. Na kipofu yule, jina lake ndilo Bartimayo, aliposikia Yesu yu karibu, kwa imani akaomba, akapona kwa neema. Nafurahi kwa kuimba: “Yesu yeye yule leo!”

 

3. Watu wote wenye dhambi na wagonjwa na maskini wanaitwa kwake Yesu kwa rehema. Uiguse nguo yake, sawa mwanamke yule, utapewa nguvu yake, kwani Yesu yeye yule!

 

4. Nimeyasikia tena jinsi alivyoombea maadui wake ju’ ya msalaba. Aliteswa kwa miiba, aliona maumivu. Ninaimba kwa furaha: “Yesu yeye yule leo!”

S.C. Kaufman, 1895
Have you ever heard the story, R.H. 442




299 JE, umelisikia jina zuri

299

1. Je, umelisikia jina zuri, Jina la Mwokozi wetu? Linaimbiwa duniani pote na katika watu wote.

Pambio:
Yesu, jina hilo linapita majina yote kwa uzuri! Ni lenye nguvu ya kutuokoa na hatia na makosa.

 

2. Linafariji moyo wa huzuni, latutia raha kuu. Katika shida na hatari huku jina hili latulinda.

 

3. Katika giza huku jina hili linang’aa kama nyota, lanipa utulivu na ‘hodari siku zote hata kufa.

 

4. Majina yote yasahauliwa, ila jina lake Yesu milele litang’aa huko juu. Yesu, jina nzuri mno!

Allan Törnberg, 1935