222 BWANA Yesu amesema
1.Bwana Yesu anasema: “Dhaifu wewe sana. Mimi ni mchunga mwema”. Na kwa hiyo namwandama.
Pambio: Yesu alikufa kwa ajili yangu, aliziondoa dhambi, furaha kubwa kwangu!
2.Pendo la Mwokozi wangu limeyeyusha moyo. Ametoa dhambi zangu na kiburi na uchoyo.
3.Sina kitu mkononi cha kunifaidia; udhaifu u moyoni, Yesu ninamlilia.
4.Mungu akisaidia nitamaliza mwendo. “Yesu alinifilia”, nitaimba huko ng’ambo.
5. Siku moja nitafika mbinguni huko juu, nitaimba kadhalika shukrani kuu.
Elvina M. Hall- T.Truvé
Min Jesus säger mig, Sgt. 419; I hear the Saviour, R.H. 198