15 MUNGU moto wako uniutumie

1. MUNGU, moto wako uniutumie, Ninangoja nguvu yako! Nipe na uzima na upendo wako, Unijaze, E’Mwokozi wangu!.

 

2. Teketeza usiyopenda, Nisafishe kati’ damu! Na karibu yangu uivunje tena, unionyeshe, Yesu, niwe safi.

 

3. Unilinde, Yesu sikuasi tena unifunge kwa pendo! Mimi ni dhaifu, unitunze kwako ‘uniongoze kwa mkono wako.

 

4. Huko juu kwako tutaona raha, na huzuni itakwisha. Nyimbo za shukrani zitajaza mbingu; utukuzwe, Yesu, Mkombozi

 




19 MUNGU tunangoja wote Roho yako ‘Takatifu

19

1. MUNGU tunangoja wote Roho yako ‘takatifu, Tunaomba kwa imani “Umtume hapa kwetu!

 Refrain : Mungu wetu, Mungu wetu, Umimine Roho yako, mioyoni mwetu, Bwana utimize kazi yako!

 

2. Washa moto wako tena, ndani ya mioyo yetu, Hata vyote vya majani vitateketea sana!

 

3. Utakase roho zetu, Na kiburi uivunje! Wewe U mfalme wetu, utawale watu wako!

 

4. Utujaze siku zote Pendo lako kubwa, Mungu! Sisi tuwe nyumba yake, Roho yako takatifu!

 

5. Na karama zake Roho utuzigawie Bwana! Na wangonjwa uwaponye, Wote wakuone Mungu!

 

 




35 NIMEFIKA kwake Yesu

35

1. Nimefika kwake Yesu, Na rohoni mwangu sasa, jua lake la neema linang’aa kila siku.

Pambio:
Roho yangu inaimba, nimefunguliwa kweli. Nimekaribia Yesu, ninaimba kwa furaha.

2. Pepo za neema yake zinavuma ndani yangu, na mawimbi ya wokovu yananijaliza sasa.

3. Sasa Bwana Yesu Kristo amefanya kao kwangu. Nimepewa mfariji, Roho ya ahadi yake.

4. «Siku roho afikapo mtajua kwa hakika kwamba ninakaa kwenu», hivyo Yesu alisema.

5. Kweli, amefika kwetu, sasa yumo ndani yetu. Ujitoe kwake Mungu, aioshe roho yako!

6. Yesu atakapokuja katita utakatifu, nitafananishwa naye, nitamshukuru sana.

Pambio:
Zitakuwa nyimbo nyingi tuta’poingia mbingu, na milele tutaimba na kusifu Mungu wetu.

Werner Skibsted




282 UKIONA kiu sana ujalivu

 282

1. Ukiona kiu sana ujalivu wa Mwokozi, roho yake safi pia, liamini neno la babako na atakujazi, nawe utashangilia.

Pambio:
Atakujaliza hata utashiba. Bwana Yesu akuita: “Njoo bila ‘sitasita!” Atakujaliza hata utashiba Roho na uwezo wake.

 

2. Vichukue vyombo vyako, uvioshe safi sana kisimani pa Golgotha! Afadhali kujitoa lote kwa Mungu Bwana, na imani itaota.

 

3.Na mafuta ya neema hayakomi. Asifiwe! Tunakuwa na shukrani! Anataka kumimina Roho ya ahadi yake. Mpokee kwa imani!

Leila Morris, 1922
Are you looking for the fulness, R.H. 214




294. UTUME Roho yako juu yetu

294

1. Utume Roho yako juu yetu kama ulivyofanya hapo kale!
:/: Uwashe moto wako ndani yetu, tusiwe watu wa uvuguvugu! :/:

 

2.Utume Roho yako juu yetu kama ulivyofanya siku ile.
:/: Mtume Petro alipohubiri katika nyumba yake Kornelio! :/:

 

3.Utume Roho yako juu yetu, utupe nasi Pentekoste yetu!
:/: Maelfu wenye dhambi waokoke, na neno lako lienee pote!:/:

 

4.Utume Roho yako juu yetu! Mikono yako uinyoshe sasa,
:/: ishara za ajabu zifanyike, wagonjwa uwaponye kati yetu! :/:

 

5.Uwaamshe waliosinzia, waliochoka huku safarini!
:/: E’ Bwana utujie kama kale ulivyowabariki watu wako! :/:

K.G. Sjölin, 1906