3 KISIMA safi sana chatoka msalaba

1. Kisima safi sana chatoka msalaba, Kimetufungukia, chatusafisha vema.
Twaweza kusikia sauti yake Yesu: ‘’Unifuate sasa kwa kiti cha neema!’’

Refrain:

Kisima cha msalaba, Damu ya Yesu Kristo, Chatusafisha sisi
sote na dhambi na hatia.

 

2. Ufike, mwenye dhambi, krisima ni karibu! Uache dhambi zako,
upumzike hapa! Katika damu yake kabisa utapona,
Tazama msalaba, kisima kitokako!

 

3. Kisima hicho safi cha damu ya Mwokozi kinatutia
afya na nguvu ya kushinda. Mfalme wetu, Yesu, tumhimidi tena!
Furaha yetu yote ni kushukuru Mungu!


 




27 UNA uhodari leo wakumufwata Yesu hata ukichekwa sana

27

1. Una uhodari leo wa kumfuata Yesu, hata ukichekwa sana na kuteswa duniani?

 

2. Una uhodari leo kuwa mtu wake Mungu? Ukiona haya sana, kisha utaona nini?

 

3. Mji unaonekana ukijengwa mlimani, hivyo na imani yetu inadhihirika sana.

 

4.Ukipenda Yesu na kuliko vitu vyote, unataka kumkiri, mbele ya wenzako huku.

 

5. Chuki au ‘pendeleo kwako kitu bure tena, watafuta siku zote sifa zake yesu Kristo.

 

6.Ujihoji nafsi yako ukitaka kuokoka! Uliekataa Mungu, tubu dhambi zako leo!

 

7. Umsihi masamaha, akuokoe ‘kati damu! Omba uhodari tena wa kumfuata Yesu!

 

8. Uchague Yesu leo, uwe mfuasi wake! Ukitwaa msalaba utaipokea taji!

 

Lina Sandell-Berg, 1859




179 SIKU moja mavuno yataisha kabisa

179

1. Siku moja mavuno yataisha kabisa, baada ya hayo hukumu.
Jua litazimika siku hiyo ya mwisho, na hutasikia injili

Refrain:
Atakusanya ngano kwa furaha ghalani bali makapi yote yatatupwa motoni rafiki utakuwa wapi

2. Mahubiri na nyimbo za wokovu wa mungu zitakaponyamaza huku,
uliyelikataa neno zuri la mungu, utakaa wapi milele

Refrain:
Atakusanya ngano kwa furaha ghalani bali makapi yote yatatupwa motoni rafiki utakuwa wapi

3. Watu wote wa mungu wafikapo mbinguni kukaa pamoja na yesu,
wataimba kabisa kwa sauti nguvu kumshangilia mwokozi

Refrain:
Atakusanya ngano kwa furaha ghalani bali makapi yote yatatupwa motoni rafiki utakuwa wapi


[youtube https://www.youtube.com/watch?v=O7D8fB3IyJs?feature=oembed&w=500&h=281]

 

 




188 WENGI wakasema: ‘Bado’

188

1. Wengi wakasema: “Bado”, walipoitwa na Mwokozi, lakini tena wakaona wamechelewa kuokoka.

Pambio:
Njoo mbio, njoo mbio, Yesu akuita leo! Njoo mbio, njoo mbio, usichelewe, ndugu yangu!

 

2.Nawe usemaye: “Bado”, unapoitwa naye sasa, rafiki, labda utakuta mlango umekwisha fungwa.

 

3. “Bado leo”, alisema kijana ‘moja kwa ujinga. Usiku alikufa mara, na akaenda hukumuni.

 

4. “Bado leo”, wamwambia rafiki yako bora, Yesu, Ataondoka kwa huzuni, utafanyaje bila yeye?

 

5. “Bado leo”, ukumbuke ni neno la hatari kwako! Waweza kupotea pia, kukosa kuingia mbingu.

Emil Petersson, arr.




194 USIKIE Bwana Yesu anakuita leo

194

1. Usikie Bwana Yesu anayekuita leo! Aliteswa, alikufa kwa ajili yako wewe.

Pambio:
Usikie Bwana Yesu! Anabisha mlangoni. Umfungulie moyo, umkaribishe sasa!

 

2. Siku zote ulicheza, kupendeza mwili wako; ulimsahau Yesu, naye alikufilia.

 

3.Unasema: “Nitakuja kusikia neno lake”. E’ rafiki, ukumbuke, unaweza kufa leo!

 

4. Yesu akuita leo kwa neema na upendo. Leo siku ya wokovu, umfungulie moyo!

 

5. Tunampa Bwana Yesu moyo na wakati wetu. Yeye ni Mfalme wetu wa milele na milele.

 

C.C. William/ D.W. Whittle, 1878
Have you any room for Jesus, R.S. 122; R.H. 362




195 TUNASIKIA leo habari

195

1. Tunasikia leo habari, inawaita watu wafike; watu wa hapa, watu wa mbali, wote wapate sasa wokovu!

 

2. Mtu wa dhambi uje upesi, Yesu angoja kukuokoa! Tena kwa nini unachelewa? Leo ni siku ya kuokoka.

 

3.Ulikimbia Yesu Mwokozi aliyekukomboa kwa damu. Usikimbie mbali zaidi, ila urudi, uje upesi!

 

4. Katika dhambi hutaiona raha halisi, hata kidogo. Yesu mwenyewe atakujaza raha ya kweli ndani ya roho.

 

5. Mtu wa heri katika shida, katika mambo yote ya huku, ni hali ya mkristo wa kweli, mtu wa heri hata milele.

T. Joseph Grytzell, 1891

[youtube https://www.youtube.com/watch?v=311WlZiXlNA?feature=oembed&w=500&h=281]




196 USIEIFANYA bidii kabisa

196

1. Usiyefanya bidii kabisa, hutaingia mbinguni. Uikinge roho kwa neno la Mungu, usipotee milele! Njia ni nyembamba na mlango ‘dogo, ujitahidishe kuingia humo! Ukubali leo wokovu wa Mungu ili ufike mbinguni!

 

2. Vizuio vingi katika safari, mwovu anakujaribu. Uvishinde vyote vinavyozuia, vyote katika dunia! Usimfuate kila aitaye, ungeweza kupoteza roho yako! Bwana Yesu anakupenda daima; ujitahidi kabisa!

 

3. Pasipo imani huwezi kufika hata bandari salama wala kuingia katika uzima; hilo ni neno la Mungu. Kwa imani tupu utaokolewa, usikie sasa neno la wokovu! Tubu dhambi zako, amini Mwokozi; hiyo ni njia, hakika.

 

4. Mungu anaita, wo wote wafike, waupokee uzima! Atakupa nawe hazina ya mbingu, ukitafuta kwa kweli. Mungu Baba anapenda roho yako, Yesu anataka kuokoa wewe, Roho ‘takatifu anakuamsha.

 

Ukiitika u heri! T. Lars Linderot, 1798




198 E’MTU mwenye kiu

198

1. E’ mtu mwenye kiu, ufike kwake Yesu, :/: upate maji ya uzima, hutaona kiu kamwe!

Pambio:
:/: Njoo kwa Yesu, uyanywe maji hai! Ufike, na utapewa uzima na uhodari!

 

2.Na tazama, ndugu wengi wamekwisha kunywa! :/: Ni heri kubwa, maji hayo hayatakauka kamwe! :/:

 

3.Na wewe unywe pia, upate nguvu sana! :/: Tumia katika shindano upanga wa neno lake! :/:

 

4.Na mwendo wa imani uta’poumaliza, :/: utayakunywa maji bora m kwa Mungu mbinguni juu. :/:

 

T.B. Barrat




199 NJONI wote muteswao

 199

1. Njoni wote mteswao! Wote wenye sikitiko kwa ajili ya makosa, mje sasa kwa Mwokozi! Kwake mtaona raha, utulivu na amani. Matulizo mioyoni mtapata kwake Yesu.

 

2.Hataacha sikitiko kulemea moyo wako; Yesu ni mchunga mwema, akuficha mazizini. Pendo lake lina nguvu, huchukua masumbuko, hufariji roho yako, hukutwaa kwake Mungu.

 

3. Yesu kama nyota nzuri ing’aayo asubuhi, mtu amfuataye ataona njia wazi. hata nyota za mbinguni zikiteketea zote, nyota hiyo ya milele haitazimika kamwe.

 

Tune: Who can cheer the heart like Jesus, R.H. 518; MA. 490




201 NJO mwenye huzuni nyingi

201

  1. Njoo, mwenye huzuni nyingi! Yesu anakungoja. Uje, atoe mzigo wako, ata’okoa wewe!

Pambio
Njoo, uliye na huzuni! Njoo kwa Mungu wa neema! Roho wa Mungu anakuita, Yesu anakungoja.

 

2. Njoo, mwenye makosa mengi! Yesu anakungoja. Kwake neema na upendo tele! Ata’okoa wewe.

 

3. Njoo, leo uache dhambi! Yesu anakungoja. Ukilemewa moyoni mwako, uje kwa Yesu mbio!

 

4. Njoo, sasa, E’mwenye dhambi! Yesu anakungoja. Na ukitaka kumfuata, ata’okoa wewe.

Georg Fr. Root




202 NJOO kwa Yesu Mwokozi

202

1. Njoo kwa Yesu Mwokozi, unayeteswa rohoni! Damu iliyomwagika itakuosha kabisa.

Pambio:
Njoo kwa Yesu Mwokozi, naye atakuokoa! Ulimwenguni ni dhiki, kwake ni raha halisi.

 

2. Mbona kukawa dhambini bila uzima wa Mungu? Uje upesi kwa Yesu ili upate amani!

 

3. Saa zapita upesi, hazitarudi kabisa. Bado kidogo na tena utapelekwa kuzimu.

 

4. Yesu atamchukua bibi-arusi mbinguni, na tutaimba milele sifa za Mwana-kondoo.

Pambio
Huko karibu na Yesu, mbali ya mambo ya nchi, huru na heri rohoni nitafurahi milele!

T.B. Barrat




203 HATUA moja kati ya wewe na Mwokozi

203

1.Hatua moja kati ya wewe na Mwokozi. Wakawilia nini? Ufike kwake leo!

Pambio:
Hatua moja, hatua moja, njoo akungoja! Njoo kutubu dhambi, atasamehe zote! Usikatae tena wokovu wake Mungu!

 

2.Hatua moja mbele, anakungoja sasa. Amini neno lake, na utapata raha!

 

3.Hatua moja mbele, uzima uta’ona. Siku si nyingi huku, ‘jitoe kwake Mungu!

 

4.Hatua moja mbele, kwa nini kukawia? Omba: E’ Bwana Yesu, unipokee sasa!

Fanny J. Crosby




204 PENDO la Mwokozi kubwa mno

204

1. Hatua moja kati ya wewe na Mwokozi. Wakawilia nini? Ufike kwake leo!

Pambio:
Hatua moja, hatua moja, njoo akungoja! Njoo kutubu dhambi, atasamehe zote! Usikatae tena wokovu wake Mungu!

 

2. Hatua moja mbele, anakungoja sasa. Amini neno lake, na utapata raha!

 

3. Hatua moja mbele, uzima uta’ona. Siku si nyingi huku, ‘jitoe kwake Mungu!

 

4. Hatua moja mbele, kwa nini kukawia? Omba: E’ Bwana Yesu, unipokee sasa!

Fanny J. Crosby




205 YESU Mwokozi aita kwapendo mimi na wewe na wote

205

1. Pendo la Mwokozi kubwa mno! Yesu akuita, ufike kwake sasa!

Pambio:
:/: Anangoja, anabisha, ufungue!:/:

 

2. Amengoja wewe siku nyingi, analia sana juu ya dhambi zako.

 

3. Kwa huruma nyingi akuita. ‘Geukie Mungu, anakungoja sasa!

 

4. Yesu atakupa raha kubwa na uzima tele ulio wa milele.

Armée du Salut.




206 RAFIKI yangu tazama

206

1. Rafiki yangu, tazama, wapita njia ya wapi? Milele, je? utakaa wapi ukikataa Mungu?

Pambio:
Ujiandae sasa, utakutana na Mungu! Lazima uwe tayari
kwa sababu utamuona!

 

2.Dunia haina raha, amani wala salama. Fahari yake ikikuloga, utapotea njia.

 

3. Lo! Yesu anakuita! Kwa nini unachelewa? Ushike njia ufike kwake! Ataja jina lako.

 

4.Uache haya na hofu, Mwokozi anakupenda! Kwa damu alikomboa wewe, anakutaka sasa.

 

5.Ikiwa unachelewa kupatanishwa na Mungu, utamkuta Mwokozi kama mwamuzi mwenye haki.

Oscar Hallof, 1921




207 UMGEUKIE Mwokozi

207

1.Umgeukie Mwokozi, jitenge na ovu na dhambi! Babako angoja ufike; usiangamie milele!

 

2. Kijana, unafurahia maisha na mambo ya nchi. Baada ya muda kitambo utahukumiwa na Mungu.

 

3. Kwa nini kujiangamiza katika tamaa za huku? Usijipoteze dhambini! Dunia isikuharibu!

 

4.Umkimbilie Mwokozi, atakupokea kwa pendo, na utaokoka hakika kwa nguvu ya damu ya Yesu!

 

5. Walio mbinguni waimba, wanayo mavazi meupe; hutaki sehemu pamoja na wao nyumbani mwa Baba?

 

6. Je, mwisho utaona wapi mahali pa kujisitiri? Dunia itakapochomwa utakosa makimbilio.

 

7. Ujipatanishe na Mungu, na usichelewe, rafiki! Ukimkataa Mwokozi, utatupwa nje gizani.

 

8. Chagua pasipo kukawa! Mwokozi atakupokea. Angoja ufike kutubu; atakutakasa kwa damu.




211 NJOO kwa Yesu

 211

1. Njoo kwa Yesu, usishangae! Akuonyeshe njia ya mbingu. Msikilize, anakusihi: Mtu wa dhambi, njoo!

Pambio:
Heri, heri, tutakusanyika kwake Mungu kwa furaha kuu! Shida na shaka hazitakuwa kwetu mbinguni juu.

 

2. Yesu aita, wote wafike, atatuliza wenye huzuni, kuwatolea pendo na raha. Usikiaye, njoo!

 

3. Sasa wakati wakuokoka, uje upesi, umkubali! Mwenye amsikitiko na dhambi, njoo kwa Yesu sasa!

G.F. Root, 1870
Come to the Saviour, R.S. 123; R.H. 308




212 SAUTI ya Yesu niliisikia

212

1. Sauti ya Yesu niliisikia, kwa pendo aliniambia: “Ufike, nataka kukusaidia, nangoja, nangoja, ufike!”

Pambio:
Njoo kwa Yesu, ufike upesi, uupokee wokofu wa Mungu! Mbona kukawa dhambini, rafiki? Yesu anakuita, njoo!

 

2. Ukiwa na hofu kufika kwa Yesu, uliye na dhambi rohoni, kumbuka ya kuwa huruma ni tele; ufike kwa Yesu, angoja!

 

3.Ukiwa maskini, dhaifu kabisa, Mwokozi anakufahamu. Anakuambia: ” Pokea neema, uache mzigo wa dhambi!”

 

4. Na kama nilivyo ninamfikia Mwokozi aliyenipenda. Ninaupokea wokovu na raha; kwa shangwe ninamshukuru!




213 KAMA unataka kuwa mtu wake Yesu

213
1. Kama unataka kuwa mtu wake Yesu, kama unataka kufuata yeye, kama unataka yeye akusaidie: Mpe Yesu moyo wako!

Pambio:
Ataondoa dhambi zako zote, na utaipokea nguvu yake! Ukiokoka utaona kwamba ni vizuri kufuata Yesu kweli.

 

2. Kama unataka kuwa mtu mwenye heri, ufungue moyo, Yesu aingie! Kama unataka utulivu na faraja, mpe Yesu moyo wako!

 

3. Kama unataka kumtumikia Yesu na kuifuata njia yake hapa, kama unataka kuingia huko mbingu: Mpe Yesu moyo wako!

C.S. Nusbaum
Would you live for Jesus. R.S. 574




214 NAMTAFUTA mwana wangu

214

1. Namtafuta mwana wangu, mtoto yu wapi leo? Alienifurahisha mbele, ningali ninampenda.

Pambio:
Mwanangu yu wapi leo? Mwanangu yu wapi leo? Mwanangu, urudi, ninakutafuta, mwanangu, mpendwa wangu!

 

2. Uliyekuwa safi sana katika utoto wako, uliichafua roho yako kwa dhambi na njia mbaya.

 

3. Ninatamani kukuona katika usafi tena, na kukusikia ukiomba na kumshukuru Yesu.

4. Nitafutie mpotevu kwa pendo na tumaini! Unisalimie mwana wangu, ya kwamba ninamngoja!

Robert Lowry, 1877
Oh, where is my wandering boy to-night.




216 NAFASI ingaliko arusini

216

1. Nafasi ingaliko arusini ita’yokuwa kwake Mungu Baba. Njoo kwake, nafasi ingaliko!

 

2.Njiani mwako jua linakuchwa, jioni inakaribia sasa. Njoo mbio, nafasi ingaliko!

 

3. Karamu ya arusi ni tayari, na Bwana anakualika wewe. Njoo mbio, nafasi ingaliko!

 

4. Wanaingia watu wengi huko, ufanye hima, uingie nawe! Njoo mbio, nafasi ingaliko!

 

5. Tazama, lango limefunguliwa, neema gani: Utakaribikshwa! Njoo mbio, nafasi ingaliko!

 

6.Ufike mbio, utaona heri, Yesu atoa wingi wa neema! Njoo mbio, nafasi ingaliko!

 

7.Je, utaona shangwe ya mbinguni? Bwana arusi akungoja sana. Njoo mbio, nafasi ingaliko!

 

8.Uliyesitasita unaitwa, ujiazimu kuja kwake Mungu! Njoo mbio, nafasi ingaliko!

 

9.Ukichelewa, lango litafungwa, na utalisikia neno hili: “Ondokeni! Sikuwajua ninyi!”

H. Bonar




228 WAKATI wa utoto wako

228

1. Wakati wa utoto wako, hujapoona shida bado, sauti ilikuambia: “Unipe sasa moyo wako!”

Pambio:
Wajua ni nani huyu anayekuita sasa? Ni Yesu, rafiki yako; anakuita: ” Njoo kwangu!”

 

2. Na katika ujana wako wausikia mwito wake, na jinsi utakavyoshinda shetani akikujaribu.

 

3. Wakati wa uzee wako dhambini ukiendelea hata kukaribia kufa, Mwokozi akuita tena.




233 TAZAMA Mwokozi aliekufilia

233

1. Tazama Mwokozi aliyekufilia ili wewe upate uzima! Tazama, kwa pendo atakusaidia, usidumu dhambini daima!

Pambio:
Yainue macho! Tazama Mwokozi aliyekufilia, ili upate uzima!

 

2. Mwokozi alisulibiwa ju’ ya mti ili sisi tupate wokovu. Alitukomboa kwa damu yake safi, kwate yeye twapata wongofu.

 

3. Hakuna majuto yaweza’ kutuponya, ila damu ya Yesu Masiya. Ufike kwa Yesu apate kukuonya jinsi yaondokavyo hatia!

 

4. Rafiki, waitwa na Mungu kwa wokovu, anataka ufike upesi. Kwa nini kukawa, ufike bila hofu, uondoke katika hatari!

 

5. Ufike, pokea uzima wa milele, Bwana Yesu ali’tuletea! Karama ya mbingu ni tumaini letu, ipokee na hutapotea!

Amelia M. Hull, 1860




234 UTUKUFU wa mbinguni niwa heri na amani

234

1. Utukufu wa mbinguni ni wa heri na amani, dhambi hazitakuwamo. Vitu vyote vilivyomo ni vya tunu na thamani, dhambi hazitakuwamo.

Pambio
Dhambi hazitaingia mbingu ya utakatifu. Ukidumu mwenye dhambi bila kutakaswa huku, hutaingia mbinguni.

 

2. Kama unatumaini kufikia nchi ile na kuona Bwana Yesu, utafute utakaso na kupata moyo safi! Dhambi hazitakuwamo.

 

3. Unaweza ‘tenda dhambi na kukana Bwana Yesu, walakini ukumbuke: Dhambi zako zitafunga lango la mbinguni, kwani dhambi hazitakuwamo.

 

4. Na ukiwa mkaidi hata sa’ ya kufa kwako, utaitwa hukumuni, na utaambiwa huko: “Ondokeni siwajui!” Dhambi hazitakuwamo.

Pambio:
Ukitaka kufikako mbingu ya utakatifu, tubu sasa, hacha dhambi, utafute moyo safi, na utaingia mbingu!

C.W. Naylor