160 AHADI zote za Mungu wetu zanasimama hata milele

160

1. Ahadi zote za Mungu wetu zinasimama hata milele. Milima yote ikianguka, ahadi hazipunguki.

Pambio:
Ahadi zake zinasimama, hazipinduki hata milele. Ikiwa nyota zingezimika, ahadi zake zinadumu.

 

2. Ahadi zake zinasimama katika shida, katika giza. Na nikichoka kwa vita kali, ahadi hazipunguki.

 

3. Ahadi zake zinasimama katika homa, katika kufa. Nafarijiwa na Baba yangu, ahadi hazipunguki.

 

4. Ahadi zake zinasimama; nitaamshwa katika kufa. Kwa Baba nitapokea taji; ahadi hazipunguki.

Johan Holmstrand, 1924




163 AHADI zote za Mungu zinasimama kweli

163

1. Ahadi zote za Mungu zinasimama kweli, na zilitiwa muhuri kwa damu yake Yesu.

Pambio:
Mbingu zikiondoka, nchi ikitoweka, ‘aminiye ‘taona: Ahadi zinadumu.

 

2. Fanya kama Ibrahimu: Uangalie juu! Nyota ukizihesabu, imani itaota.

 

3. Katika giza njiani tutaamini tu. Muda kitambo, na tena jua litaangaa.

 

4. Watu wakitusumbua, tutaamini tu. Yesu atusaidia majaribuni pote

 

5. Rafiki wakituacha, tutaamini tu. Yesu, rafiki mkubwa, atabaki daima.

 

6. Katika mambo yo yote tutaamini tu. Tutaviona mbinguni tulivyoviamini.

Lewi Pethrus, 1913




285. NENO la Mungu ndani ya Biblia

285

1. Neno la Mungu ndani ya Biblia limetolewa na Mwenyezi Mungu. Biblia yetu inatuambia: Njoo kwa Yesu, Mkombozi wetu!

Pambio:
Neno la Mungu tulilolipewa, njia ya mbingu limetuonyesha; nuru gizani ya kutuongoza katika mwendo wetu kwenda mbinguni.

 

2. Siku za giza zinakaribia, kama walivyosema manabii. Biblia yetu itatuangaza na kutuonya njia hata mwisho.

 

3. Katika neno la Biblia yetu tunaupata utajiri wote. Mbingu na nchi zitaangamia, neno la Mungu litashinda yote.

Thoro Harris, 1874-1955