65 HUKO ju’ ya nyota zote kuna chi yenye mema

65

1. Huko ju’ ya nyota zote kuna nchi yenye mema, Mji wake ni Yerusalemu; Dhambi haitakuwamo, wala kufa na huzuni, Kwake yesu nitapata kao.

Pambio:
Sikitiko na machozi hayatakuwako huko, Wala giza au vita ya dunia. Huko hatutayaona mambo ya kutuumiza. U Yerusalemu ‘takatifu!

 

2.Nifikapo mji huo nitaona Yesu kwanza, aliyechukua dhambi zangu. Nitaona uso wake, nitamshukuru yeye aliyeniweka huru kweli.

 

3.Huko nitaona tena jeshi la walioshinda kwa imani huku duniani, na pamoja nao wote nita’sifu Mungu sana juu ya neema yake kubwa.




66 WAKRISTO wa nchi zote watakusanyika huko kwa Yesu

66

1. Wakristo wa nchi zote watakusanyika huko mbinguni kwa Yesu, mezani pake, kati’ ufalme wake; kuona uzuri wake, kujazwa neema yake. Wataimba huko ju’ milele na milele.

Pambio:
Watoka bahari zote, watoka katika shida, watoka milima, watoka mabonde kufika kwa Mungu Baba, kuvikwa mavazi safi, kuona Mwokozi wao, yeye ali’wafilia ju’ ya msalaba.

 

2. Watakusanyika wengi walikotoka huku. Mateso na kufa, shida na giza hawata’ona kamwe. Ya kale hayatakuwa, lo! yote ni mapya huko! Itakuwa raha tu pamoja na faraja.

 

3. Tazama mlango huko uliokufunguliwa, na kuna mahali Yesu aita: « Njoo nyumbani kwangu wenzetu waliofika wanatungojea huko, malaika wanaimba kukukaribisha. Amanda Sandbergh




68 MBINGUNI kwa Mwokozi wangu mwema nitaamka asubuyi moja

68

1. Mbinguni kwa Mwkozi wangu mwema nitaamka asubuhi moja, Nitayaona majeraha yake, sauti yake nitaisikia.

 

2. Makao ya milele ni tayari, ali’waandalia watu wake. Tutamsifu Yesu sana huko, aliyetuokoa na hatari.

 

3.Na nyimbo za wokovu zinaimbwa mbinguni mbele ya Mwokozi wetu; tungesikia huku nusu ndogo, vitani tungepata ushujaa.

 

4. Lakini Yesu yupo nasi leo, usiku kama moto mbele yetu. Na neno lake, ni upanga wetu, ahadi ni safina ju’ ya maji.

 

5. Tungoje Yesu siku chache tena! Twakaribia mwisho wa safari. Tungoje asubuhi huko juu! Atatukaribisha Bwana Yesu!

Charlotte af Thibell




69 JE, Tutaonana tena huko ng’ambo ya Yordani

69

1. Je, tutaonana tena huko ng’ambo ya Yordani, na pamoja na wakristo ‘ona raha ya milele?

Pambio:
Tuonane, tuonane huko ng’ambo ya bahari! Tuonane kwa furaha, huko shida ikomapo!

 

2. Je, tutaonana tena, ba’da ya dhoruba zote huko katika bandari ya salama na amani?

 

3. Je, tutaonana tena kati’ mji wa dhahabu, Penye mto wa uzima nayo miti ya matunda?

 

4. Je, tutaonana tena na kusifu Mungu wetu miongoni mwa wakristo waimbao huko juu?

 

5. Tutaona na wapenzi waliotuacha huku? Je, tutawaona wote katika makao meme

 

6. Tutaona Bwana Yesu katika kutano huko, tutakaribishwa naye katika karamu kuu.

Th. Hastings




70 KUNA mji uko juu

70

1. Kuna mji huko juu, umejengwa naye Mungu, humo kuna mto ‘moja wenye maji mazima kabisa.

Pambio:
Tutakusanyika huko kwa raha penye mto mwema sana, tutakusanyika na wakristo penye mto wa maji mazima.

 

2.Huko pwani nchi nzuri, bila dhambi na huzuni, tutaimba nyimbo mpya, nyimbo njema ‘kusifu Mwokozi.

 

3. Kama twamwamini Yesu, kama hatufichi dhambi, kama moyo ni mweupe, tutafika mtoni pa mbingu.

 

4. Tu karibu ya kufika na kuona mto ule, Mungu atatupa raha na kutustarehesha daima.

R. Lowry
Shall we gather at the river, R.S. 664 




75 NILIE msafiri

75

1.Niliye msafiri, mgeni duniani; sioni kwangu hapa, ni huko ju’ mbinguni. Ninatamani nami kukaa siku zote pamoja naye Baba katika utukufu.

Pambio:
Kwangu mbinguni, kwangu, uzuri wa binguni wapita yote huku.

 

2. Mwokozi yuko huko, rafiki yangu mwema, aliyenikomboa na ku’chukua dhambi. Na hata nikiona furaha siku zote ningali natamani makao ya mbinguni.

 

3.Na nikipewa huku vipawa vya thamani, na wakiimba nyimbo za kunifurahisha, rafiki wangu wote wakipendeza mimi, ningali natamani makao ya mbinguni.

 

4.Upesi nitaona kifiko cha mbinguni, Mwokozi wangu Yesu atanikaribisha; Na huko nitaona nilivyotumaini, kinubi nita’piga kumshukuru Yesu.

Lina Sandell-Berg, 1868
Home, home, sweet home


[youtube https://www.youtube.com/watch?v=RMNKXUgJql4?feature=oembed&w=500&h=281]




77 NAIFUATA njia ya ku’fikia mbingu

77

1. Naifuata njia ya kufikia mbingu na mji mwema ule alio’jenga Mungu. Ninasafiri sasa kutoka duniani nifikie nchi hiyo ya raha na uzima.

Pambio:
Naifuata njia ya ku’fikia mbingu na mji mwema ule alio’jenga Mungu.

 

2. Sijauona bado uzuri wake bora wa mji wa mbinguni, usio na machozi; lakini siku moja, kwa shangwe ya milele nitamsifu Yesu katika mji ule.

 

3. Nifikapo mjini, mlango wake wazi, na hapo malaika watanikaribisha; shindano la dunia halitakuwa huko, na nitaona raha milele na milele.




80 ZITAKAPOTIMIA siku zahuduma yangu nitaona asubuhi ya uzima

80

1. Zitakapotimia siku za huduma yangu, nitaona asubuhi ya uzima. Huko juu mbinguni nitamwona Bwana Yesu, Na karibu yake nitaisikia.

Pambio:
Nitamtambua yeye, na karibu ya Yesu nitakaa. Nitamtambua yeye kwa alama za majeraha yake.

 

2.Itakuwa furaha kuona uso wake, na uzuri utokao macho yake. Moyo utafurika na uheri na furaha, ju’ ya kao aliloniandalia.

 

3.Na walio mbinguni wananingojea kwao, nakumbuka siku tulipoachana. Wataimba kabisa kunikaribisha huko, walakini nitamwona Yesu kwanza.

Fanny J. Crosby
When my life-work is ended, R.S. 364




82 NINAJUA chi nzuri

82

1. Ninajua nchi nzuri, huko Mungu alifanya nyumba na makao kwetu; natamani kufikako.

Pambio:
Mbinguni, kao la malaika! Mbinguni, vyote vinamulika! Mbinguni Mungu atualika tukusanyane mbinguni kwake!

 

2. Katika safari yangu ninajiuliza sana kama nami nitafika penye Mungu ndie jua.

 

3. Kwa neema yake kubwa nitakaa kwake Mungu, Bwana Yesu atanipa taji nzuri ya uzima.

 

4. Sasa ninapiga mbio, nifikie nchi hiyo ya uzima na furaha, nchi ya tamani yangu!

Eric Bergqvist, 1903




83 NINAJUA nchi uko juu

83

1. Ninajua nchi huko juu, hapo Mungu alijenga mji, na aita ‘moma moja kwake, waliomaliza mwendo huku.

Pambio:
Shida, kufa na huzuni hazitakuwapo huko. Yesu atafuta kila chozi, tutaona shangwe, nayo tele.

 

2. Huko hawataingia kamwe wenye dhambi, wala cha kinyonge, E’ rafiki, ujihoji leo kama wewe utaona mbingu!

 

3. Utazame, mto ungaliko uwezao kusafisha sana! Ujioshe kati’ damu safi ya Mwokozi wetu Yesu Kristo!

 

4. Nafurahi kwani ninajua kao langu liko huko juu, natamani sana kufikako. Njoo, Yesu, unitwae mbio.

Mathilde Wiel-Öjerholm




84 NINAKUMBUKA sayuni

84

1. Ninakumbuka Sayuni, nchi ya heri mbinguni, bahari kama kioo na’furahia rohoni. Nyuma kimeta cha nuru Naona mji wa mbingu, nyimbo za nyumba ya Baba nasikiliza daima.

Pambio:
Mapambazuko mbinguni yataondoa utaji, vyote tulivyoamini tutaviona milele.

 

2. Mauti haina nguvu, Yesu a’vunja uchungu, naye aliwakomboa wote; wafalme, watumwa. Ninamtwika Mwokozi dhambi, huzuni na shida; mbavuni mwake nafasi kama bandari salama.

 

3. Kuna ‘jaribu njiani, mengi yakunizuia, na mara nyingi miiba, inaumiza miguu. Nikikumbuka Sayuni moyo huwaka kabisa, mbingu ninaitazama na ku’himiza safari.

Th. B. Barrat, 1904




85 TWAPASHA habari ya mbinguni

85

1. Twapasha habari ya mbingu, mahali pa watu wa heri, na tunatamani ku’ona ufuko wa nchi ya mbingu.

Pambio:
Sikitiko, wala shida hazitakuwapo mbinguni. Huko juu, huko juu tutashangilia milele.

 

2. Twapasha habari ya mbingu na mji mzuri ajabu, na jeshi la watakatifu waliomaliza safari.

 

3. Twapasha habari ya pendo, amani na nguo nyeupe. na raha baada ya vita, makao karibu na Mungu.

 

4. Twapasha habari ya Yesu, alituokoa na dhambi. Ingawa ni shida njiani atatufikisha mbinguni.

Elisabeth Mills, 1829




86 TUTAONA furaha mbinguni

86

1. Tutaona furaha mbinguni, ni makao ya watu wa heri. Tutakuwa pamoja na Mungu na kusifu Mwokozi wetu.

Pambio:
Tutafurahi na tutaabudu huko juu kwake Mungu. Tutafurahi na tutaabudu siku tutakapofika.

 

2. Mara nyingi furaha ya hapa yapinduka machozi machongu, walakini hazitakuwapo sikitiko na shida huko.

 

3. Kama shida na shaka zafika kuzuia safari ya hapa, tutazame daima mbinguni, huko juu ni raha yetu!

Robert Harkness




87 MWSHO wanjia ya Mungu ni mbingu

87

1. Mwisho wa njia ya mkristo ni mbinguni; Yesu ananiongoza salama. Kama shetani akinijaribu nakitazamia kifiko.

Pambio:
Kwetu mbinguni hatutatawanyika, dhambi na mateso hayatakuwapo, Na hatutaona machozi na shida, ila furaha milele.

 

2. Tutawaona walioishinda dhambi, shetani na mambo mabaya, na tutaona Mwokozi mpenzi; tutafananishwa na yeye.

 

3.Nani ataka kufika mbinguni? Yesu ni njia, uzima na kweli. Njoo kwa Yesu! Akuandalia kao la milele mbinguni.

 

4. :/: Malaika wanangoja:/: malaika wanangoja huko mbinguni! :/: Malaika wanangoja:/: kutusalimu: «karibu».




97 BADO kidogo juwa litapanda

97

1. Bado kidogo jua litapanda, siku tuta’pofika huko juu. Huko mbinguni tutapumzika na’pata raha na furaha ya milele.

Pambio:
Tutamlaki Bwana Yesu Kristo, aliyetuokoa kweli hapa chini. Huko mbinguni tutamwona yeye, tutamsifu kwa upendo wake ‘kuu.

 

2. Bado kidogo tutaona vyote vitageuka kuwa vipya tena, na hapo, Yesu, Mwokozi wetu, atatufungulia lango la mbinguni.

 

3. Safari yetu ina majaribu, tutafurahi kwa kufika mbingu. Hatutaona giza, shaka tena, Tutamshangilia Mwokozi wetu.

James Rowe




258. MIKUTANO kubwa gani mlimani

258

1. Mkutano ‘kubwa gani mlimani mwa Sayuni asubuhi ya milele? Hawa walinunuliwa tena walitakasiwa, wawe malimbuko kwa Mwokozi.

 

2.Hata kufa huku chini walikuwa waamini, walimfuata Yesu. Sasa wanaka’ mbinguni, wametoka jaribuni, wamerithi raha yakipeo.

 

3.Ukamili wa uzuri wa muziki na zaburi unatoka huko juu! Ni sauti tamu mno ya kinubi na ya wimbo kandokando ya Mwokozi wetu!

 

4. Wimbo huo ni wa nani, wa sauti ya tufani, wa kutia raha kuu? Ndio wimbo mpya ule uimbwao sasa kule ili kuhimidi Mkombozi.

 

5. Bwana, unilinganishe, na ulimi u’safishe, nami nikaimbe huko! Nipe vazi la rohoni, safi sana, la kitani lifaalo asubuhi hiyo!

Carl Boberg, 1884




259. NAFIKIRI siku tutakayofika huko kwetu

259

1. Nafikiri siku tutakayofika mbinguni huko kwetu, na malaika kwa furaha watatukaribisha.

Pambio:
Wataimba wimbo wakutupokea: “Karibuni! Karibuni wote kwetu!” Malaika wa Mungu watatulaki kwa nyimbo za furaha: “Twawasalimu! Karibu kwetu!”

 

2. Mkutano ‘kubwa umekwenda mbele na sasa uko kule. Huimba kwa sauti kuu ukimsifu Mungu.

 

3. Sisi nasi tutakusanyika huko Yerusalemu mpya, na mkutano wa wakristo utatuamkia.

 

4. Bwana Yesu naye atatupokea, atatukumbatia katika nyumba ya mbinguni iliyo ya milele.

Fredrik Engelte




260. MWENYEZI amejenga mji

260

1. Mwenyezi amejenga mji, Mfalme wa huko ni Yesu, Yohana aliouona kushuka kutoka mbinguni. Ukuta ukawa wa jaspi, na njia ya dhahabu safi. Wakati nitakapohama, nitachukuliwa Sayuni.

Pambio:
Mjini mle mtakatifu Yesu atuandalia makao. Sasa nangoja, nautamani mji mzuri kutoka mbinguni.

 

2.Na dhambi hazitafikapo, uchafu hautaingia, mateso, ugonjwa na kufa hazitakuwapo mjini. Na mle tutayasahau mashaka, ‘jaribu na vita; hatutaachana milele. Hakuna uchungu rohoni!

 

3. Mjini hatutayaona kilio na maombolezo. Na huko hatutadanganywa, haitakuwamu husuda. Na wana wa Mungu waona uzuri na utakatifu; nitakapofika mjini nitashangilia daima

 

4. Wapenzi, rafiki na wale waliomaliza safari, watashangilia kabisa kwa’jili ya damu ya Yesu. Na tutawaona mjini katika makao ya raha. Tumaini letu ni hili: Tutakusanyika mbinuni.

 

 

[youtube https://www.youtube.com/watch?v=sVng7N4UtRc?feature=oembed&w=500&h=281]




261. MSAFIRI uliye njiani

261

1. Msafiri uliye njiani, watamani nyumba ya babako. Sikiliza nyimbo za mbinguni! U karibu sana kufikako.

Pambio:
Utakuwako huko, katika mkutano wa wakristo huko mbinguni kwa raha ipitayo fahamu? Utakuako huko wakati wa kuimba wimbo mpya wa kumsifu Mwokozi siku zote?

 

2. Sikiliza sasa makengele yapigwayo huko juu kwetu, ili kutuita sisi mbele ya jioni ya maisha yetu!

 

3. Labda siku ile ni karibu nitakapokwenda, nitahama! Sitaona tena majaribu, nitajazwa kwa kumtazama.

 

4. Lango la mbinguni wazi sasa, Yesu amelifungua kwako. Utaweza kuokoka hasa, usiharibishe heri yako!

Josef Rogner, 1921




264. E’MSAFIRI jangwani

264

1. E’ msafiri jangwani, tazama juu mbinguni! Hapo utaona nyota za faraja na tumaini.

Pambio:
Huko hutayaona machozi wala shida. Mungu atatuliza msafiri mbinguni kwake.

 

2.Ukisumbuka gizani katika pepo, dhoruba, bado wakati mfupi, nuru itatokea tena.

 

3.Ukililia wapendwa waliokutangulia, utakutana na wote, hutalia machozi tena.

 

4. Na karibu na Bwana Yesu utastarehe daima, hutakumbuka mbinguni shida, kufa na sikitiko.




293. NCHI nzuri ya raha ajabu

 293

1. Nchi nzuri ya raha ajabu, kwa imani twaona si mbali. Baba atungojea sababu ametuandalia mahali.

Pambio:
:/: Tukutane sisi sote huko juu nyumbani mwa Baba!:/:

 

2. Huko juu kwa raha, amani tutaimba na kushangilia, kutolea Mwokozi shukrani kwa sababu alitufilia.

 

3. Baba wetu mpendwa na mwema kwake kuna furaha ya tele. Twamsifu kwa kuwa neema yatutosha kabisa milele.

S.F. Bennet, 1867
There ‘s a land that is fairer than day, R.S. 305; R.H. 788