15 MUNGU moto wako uniutumie

1. MUNGU, moto wako uniutumie, Ninangoja nguvu yako! Nipe na uzima na upendo wako, Unijaze, E’Mwokozi wangu!.

 

2. Teketeza usiyopenda, Nisafishe kati’ damu! Na karibu yangu uivunje tena, unionyeshe, Yesu, niwe safi.

 

3. Unilinde, Yesu sikuasi tena unifunge kwa pendo! Mimi ni dhaifu, unitunze kwako ‘uniongoze kwa mkono wako.

 

4. Huko juu kwako tutaona raha, na huzuni itakwisha. Nyimbo za shukrani zitajaza mbingu; utukuzwe, Yesu, Mkombozi

 




17 UKAE nami giza inafika!

17

1. UKAE name, giza imefika! Usiniache, Mungu, nakuomba! Unayejuwa udhaifu wangu’ Nategemea wewe, ‘kae nami

 

2. Maisha yangu ni mafupi sana, Uzuri wa dunia utakwisha. Kuna machozi, kufa huku chini, wewe Mwokozi wangu, ‘kae name!

 

4. Nakuhitaji wewe siku zote, Unayeweza sana kunilinda. Wewe shujaa wa kushinda wote, katika hali zote ‘kae.

 

5. Unionyeshe msalaba wako, Nione nuru yako kati’ giza! Na nikiishi au nitakufa, wewe, Mwokozi wangu, ‘kae name!




18 MUNGU wetu yu karibu kututia nguvu yake

18

1. MUNGU wetu Yu karibu kututia nguvu yake. Mbingu in maghubari, Tuletee mvua saa!

Refrain:
Tusikie, Mungu wetu, Tubariki saa hii! Tunangoja, tunangoja, tunyeshee nguvu yako!

 

2. Mungu wetu Yu karibu, hapa ni Patakatifu, Sisi sote tunangoja kujaliwa naye Mungu.

 

3. Mungu wetu Yu karibu, Kwa imani tunaomba: Tuwashie moto safi ndani ya mioyo yetu.

 

4. Mungu ufungue mbingu, Twalia nguvu zako! Tubariki saa hii kwa rehema zako kuu!




19 MUNGU tunangoja wote Roho yako ‘Takatifu

19

1. MUNGU tunangoja wote Roho yako ‘takatifu, Tunaomba kwa imani “Umtume hapa kwetu!

 Refrain : Mungu wetu, Mungu wetu, Umimine Roho yako, mioyoni mwetu, Bwana utimize kazi yako!

 

2. Washa moto wako tena, ndani ya mioyo yetu, Hata vyote vya majani vitateketea sana!

 

3. Utakase roho zetu, Na kiburi uivunje! Wewe U mfalme wetu, utawale watu wako!

 

4. Utujaze siku zote Pendo lako kubwa, Mungu! Sisi tuwe nyumba yake, Roho yako takatifu!

 

5. Na karama zake Roho utuzigawie Bwana! Na wangonjwa uwaponye, Wote wakuone Mungu!

 

 




20 BWANA Yesu uniongoze baharini huku chini

20

1. BWANA Yesu, uniongoze Baharini huku chini, Juu ya mawimbi mengi, Katika dhoruba kali! Bwana Yesu, uniongoze, Nakutegemea wewe.

2. Bwana Yesu, uniongoze, Utulize moyo wangu! Neno moja kwako, Marashwari baharini. Bwana Yesu uniongoze, Nipe utulivu wako!

3. Bwana Yesu uniongoze, Niyashinde majaribu! Mengi ya kunidanganya, Mengi ya kufunga macho! Bwana Yesu uniongoze, Niwe mshinadji kweli.

4. Bwana Yesu uniongoze, Siku nita’vuka ng’ambo! Nikiona woga , giza, Nipe nuru na amani! Bwana Yesu, uniongoze, Uwe nami hata mwisho!

 




21 JUU ya mbingu zote

21

1. JUU ya mbingu zote, Nyota na jua pia, Hapo yafika kweli Maombi ya mwene dua. Roho ya mwana-damu yamfikia Mungu, Huko yabisha lango na kumtafuta Baba.

2. Roho haitaona raha amani huku; Kuna bandari njema Mbinguni kwa Mungu Baba. Moyo utatulia, Nuru itatokea Tukifuata njia ya sala na maabudu.

3. Hata mototo ‘dogo mwenye kuomba Mungu, Hana la kuogopa; Kuomba kwa faa sana. Tusisahau tena, pote twendapo huku kwamba maombi yetu yafika kwa Baba.

 

Augusta Lönnborg, 1895

 

[youtube https://www.youtube.com/watch?v=dmVD--g2rQk?feature=oembed&w=500&h=281]




22 YESU KRISTO bwana wangu

22

1. YESU Kristo Bwana wangu, Una amri na uwezo za kuziondoa dhambi, Na ‘takasa roho yangu.

Refrain:
Nitolee masamaha, ‘niokoe na jaribu, unilinde hata mwisho, Unitwae kwako juu!

2. Mbele nilikuwa mwovu, nilikukataa, Yesu, Kwa hakika sikujuwa wewe na upendo wako!

3. Bwana Yesu, usamehe dhambi nilizozifanya! ‘siitike majaribu, nguvu yako inilinde!

4. Tangu sasa Wewe, Yesu, U Mwokozi na Rafiki, Nimetengwa na Shetani, Niwe wako siki zote!

 




23 NIKITAZAMA kwa imani Mwokozi wangu

23

1. NIKITAZAMA kwa imani, Mwokozi wangu, Yesu, Nawaka kwa upendo wake, Na ninavutwa kwake; Naona majeraha yake, Mikono na ubavu wake, Na humo najificha sana, Moyoni mwa upendo

 

2. Imanuel upendwaye, Nilinde sikuzote, Mpaka nihamie kwako Mbinguni mwa uheri! Milele na milele huko hapana la kunizuia Nimsifu Bwana Yesu kwa damu na ‘jereha.




25 MVUA yambingu unyeshe

25

1. Mvua ya mbingu unyeshe, kama ulivyo ahidi! Juu ya dunia yote inye kutubarikia!

Pambio
Mvua ya mbingu, mvua ya mbingu utume! Utunyeshee neema, tunakuomba, e’ Mungu!

2. Mvua ya mbingu unyeshe, ituamshe na sisi! Ju’ya vilima na bonde mvua ya mbingu ifike!

3. Mvua ya mbingu unyeshe katika dunia yote! Watu wa Mungu wapone, mbegu za roho ziote!

4. Mvua ya mbingu unyeshe, tunapokuelekea! Utujalie baraka tunakuomba, e’ Mungu!




26 NAKUHITAJI Yesu

26

1. Nakuhitaji, Yesu, Mwokozi wangu mwema, sauti yako nzuri iniletee raha!

Pambio:
Nakuhitaji, Yesu, usiku na mchana! Katika sala yangu unibariki sasa!

 

2. Nakuhitaji, Yesu, unionyeshe njia! Na unitimizie ahadi za neema!

 

3. Nakuhitaji, Yesu, uwe karibu nami, nipate kulishinda jaribu la shetani!

 

4. Nakuhitaji, Yesu, katika mambo yote, kwa kuwa bila wewe maisha hayafai.

 

5. Nakuhitaji, Yesu, njiani huku chini, nipate kuwa kwako milele na milele!

 

Annie S. Hawks, 1835-1918
I nee Thee every hour, R.H. 568




56 YESU ninakutolea vyote

 56

1. Yesu, ninakutolea vyote ninakuwa navyo, nikupende, nifuate wewe siku zote hapa!

Pambio:
Ninakupa vyote, ninakupa vyote, Bwana Yesu upendwaye, ninakupa vyote.

 

2. Miguuni pako, Yesu, ninakusujudu sasa. Ninakutolea vyote: roho, moyo na maungo.

 

3.Najitoa kwako, Yesu, nafsi yote iwe yako! Bwana Yesu, nakusihi: Niwashie moto wako!

 

4. Yesu, ninakupa vyote, unijaze Roho yako! Nisikie moto wako ukiwaka ndani yangu!

 

5. Vyote ninakupa, Bwana, viwe mali yako kweli! Na fahari ya dunia naiona ni ya bure.

J.W. van de Venter, 1896
All to Jesus I surrender,, R.S. 581




57 YESU uliye kufa kwa ajili yangu

 57

1. Yesu, uliyekufa kwa ajili yangu, ninajitoa kwako, niwe mali yako! Bwana, nivute kwako, nifaamishe pendo, niwe dhabihu hai katika shukrani!

 

2. Yesu, nafika kwako, kao la rehema; Bwana, nitie nguvu kwa neema yako! Niuchukue tena kwa radhi msalaba, ni’tumikie wewe, Mkombozi wangu!

 

3. Bwana, uniumbie moyo haki, safi, kwako niishi tena hata kufa kwangu! Niwatafute wenye dhambi na udhaifu, niwapeleke kwako, Bwana wa upendo!

 

4. Vyote ninavyo huku nimepewa nawe, ukivitaka, Bwana, uvitwae vyote! Nina urithi wangu kwako mbinguni juu, nitakuona huko kwa furaha kuu!

S.D. Phelps, 1862
Evgt. 81More love to Thee,, o, Christ, R.S. 959




59 YESU ninakutolea moyo na maisha yangu

59

1. Yesu, ninakutolea, moyo na maisha yangu, niwe mfuasi wako, Safi na mtakatifu.

Pambio:
:/: Mungu wangu, Mungu wangu, nitakase saa hii! :/:

 

2. E’ Mwokozi, nitakase, unijaze pendo lako. Na maisha yangu yote yawe yako, Bwana wangu!

 

3.Ninataka kuheshimu wewe, Mkobozi mwema; nifanane nawe, yesu, kati’ watu wa dunia!

 

4.Nikikaa kimya kwako kama yule Mariamu, nifundishwe nawe, Bwana, sitahangaika tena.

 

5. Tawi lake mzabibu, ulitunze na ‘safisha, ili kwa uwezo wako litaza’ matunda mengi!

 

Verner Skibstedt, 1930
Lord, I hear of show’rs, R.S. 277




62 MUNGU nivute kwako

62

1. Mungu, nivute kwako, karibu kwako, hata ikiwa shida ikinisukuma! Katika yote hapa ‘takuwa wimbo wangu: Mungu, nivute kwako, karibu kwako.

 

2. ‘Kiwa katika mwendo jua likichwa, giza yanizunguuka, peke yangu mimi, kwako, e’ Baba yangu, nafika, nakuomba: Mungu, nivute kwako, karibu kwako!

 

3. Unionyeshe njia yakwenda juu, nijue kupokea yote toka kwako! Unifariji sana, niimbe tena hivi: Mungu, nivute kwako, karibu kwako!

 

4. Katika mambo yote nikushukuru, majaribu’ pote nikumbuke wewe! Unifundishe hivi: Omba katika yote! Mungu, nivute kwako, karibu kwako!

5.Nikimaliza mwendo wa msafiri, Mungu utaniita kwako huko juu. Na nitaimba tena kati’ watakatifu: Umenivuta, Mungu, karibu kwako!

Sarah Flower Adams, 1841
Near, my God, to Thee, R.S. 569




63 YESU nivute karibu nawe

63

1. Yesu, nivute karibu nawe, ‘kiwa kwa shida, ikiwa kwa raha! Uliyekufa msalabani, :/: ‘nifaamishe upendo na ne’ma! :/:

 

2. Yesu, nivute, mimi maskini, sina vipaji vya kukutolea, moyo ninao wenye udhaifu, :/: Uupokee, ‘uoshe kwa damu! :/:

 

3. Yesu, nivute, nikutolee yote ninayo, e’ Bwana mpendwa, ninakuomba: Uyaondoe :/: yote yanayo nitenga na Mungu! :/:

 

4. Yesu, nivute karibu nawe hata ukomo wa vita na shida! Tena mbinguni nitakuwapo :/: karibu nawe, e’ Yesu Mwokozi! :/:

Leila Morris, 1862-1929




64 KIMYA E’moyo wangu

64

1. Kimya, e’moyo wangu, mbele za Bwana Yesu! Unahitaji sana ‘kaa daima kwake. Njia salama ipi ulimwenguni huku bila kumfuata Yesu na neno lake?

Pambio:
Uniongoze, Bwana, katika njia yako! Hata ikiwa shida nitawasili kwako.

 

2. Kimya, e’moyo wangu, omba kwa tumaini! Nuru itatokea ukiamini Mungu, na umwambie Yesu shaka uliyo nayo, atakuosha sana, atakuonya njia.

 

3. Kimya, e’moyo wangu, msikilize Mungu! akuletea nguvu, tena hekima kweli. Na ukiendelea katika neno lake, Mungu atakujaza nguvu na uthabiti.

J. Mountain, 1922




109 YESU unionye tena msalaba wako

109

1. Yesu, unionye tena msalaba wako! Huo ni kisima safi chenye kusafisha.

Pambio:
Msalaba wako, Yesu, nausifu sana. Yesu, unilinde huko hata nikuone!

 

2.Huko niliona kwanza ne’ma yako kubwa, Nuru ikafika kwangu ‘toka msalaba.

 

3. Yesu, unilinde huko, unifaamishe jinsi ulivyochukua dhambi zangu zote!

 

4.Unilinde siku zote penye msalaba, nikuone, nikupende, sasa na milele!

Fanny Crosby, 1968
Jesus, keep me near the cross, R.S. 390




110 MWAMBA ulio pasuka

1. Mwamba uliopasuka, ndani yako nijifiche! Maji yale, damu ile itokayo mbavu zako, iwe dawa ya kuponya roho yangu na ubaya!

 

2. Kazi za mikono yangu, haziwezi kukomboa. Hata ningelia sana na kutenda kazi nyingi, singeweza kuokoka, peke yako u Mwokozi.

 

3.Ndani yangu sina kitu, naushika msalaba. Uchi mimi, univike! Sina nguvu, ‘nichukue! Ni mchafu, unioshe! Wewe u Mwokozi wangu.

 

4. Kwa maisha yangu yote hata nitatoa roho, hata saa ya kuitwa mbele ya Mfalme wangu, mwamba uliopasuka, nijifiche ndani yako!

A.M. Toplady, 1776

Video hii wanaimba sauti moja ila maneno tafauti, hii ni version ya Tanzania

 




151 MWOKOZI moto safi

151

1. Mwokozi, moto safi, tunataka moto wako juu yetu! Twaomba kwako leo, Mungu: Washa moto ndani yetu, washa moto! Tazama sisi hapa leo, na tupe Roho yako, Mungu! Tupate Pentekoste yetu! Tunangoja moto wako juu yetu!

 

2. E’Mungu wetu usikie, tunaomba moto wako juu yetu! Twadumu katika kuomba: Washa moto ndani yetu, washa moto! Tunahitaji nguvu yako ili tutakasike sana na kuyashinda majaribu. Tunangoja moto wako juu yetu.

 

3. Mioyo iliyo baridi inataka moto wako juu yao. Hitaji zote tutajazwa, tukipata moto wako ndani yetu. Siwezi mimi peke yangu kushinda mambo ya shetani, lakini ninaomba, Mungu: Washa moto ndani yangu, washa moto!

 

4.Naomba moto juu yangu ili nihudumu huku kwa upendo; nauhitaji moto wako, niwe na bidii nyingi na ‘hodari. Ju’ ya madh’bahu takatifu nakuwekea moyo wangu, Mungu, washa moto, washa moto, washa moto!

W. Booth, 1894
Thou Christ, of burning, cleansing flame, R.H. 25




162 Bwana Yesu

 162

1. Bwana Yesu, uwe nami, bila wewe nina hofu, unikaribie sana, uwe kiongozi wangu!

Pambio:
Sitaona hofu tena, Yesu Kristo yu karibu. Ninataka kufuata njia yako siko zote.

 

2. Bwana Yesu, uwe nami, kwani mimi ni dhaifu; na unifariji moyo kila siku ya huzuni!

 

3. Bwana Yesu, uwe nami siku zote safarini, zikiwako shida huku au raha na amani!

 

4. Bwana Yesu, uwe nami! Nahitaji nuru yako hata nitafika mbingu, kao letu la milele!

Fanny Crosby, 1884




220 YESU wewe U mchunga wetu

220

1. Yesu, wewe u mchunga wangu, twakuomba: Utulinde! Utulishe sisi kundi lako, tukashibe neno lako!

Yesu mwema, Yesu mwema, tushibishe kwa neema! Yesu mwema, Yesu mwema, tushibishe kwa neema!

 

2. Tuongoze kwa mapito yako hata maji matulivu! Tuhuishe roho zetu huko tukajazwe uhodari!

Yesu mwema, Yesu mwema, ututie nguvu yako! Yesu mwema, Yesu mwema, ututie nguvu yako!

 

3. Yesu, uwe nasi hata mwisho, tutakapokata roho! Tupeleke katika makao uliyotuandalia!

Yesu mwema, Yesu mwema, tufikishe hata kwako! Yesu mwema, Yesu mwema, tufikishe hata kwako!

W.R. Bradbury




224 YESU mwenye pendo kubwa

224

1. Yesu, mwenye pendo kubwa, usinipitie! Katika maombi yangu unibarikie!

Pambio:
Yesu, Yesu, unisikilie! Ukiwabariki wote, usinipitie!

 

2.Ninakiendea sasa kiti cha neema; kutoamini kwangu u’ondoe vema!

 

3.Nakutegemea, Bwana, njia unionye! Roho yangu imevunjwa, Yesu, uniponye!

 

4. Wewe, Yesu, ni kisima cha furaha yetu. Nani ni mchunga mwema, ila Bwana wetu! Frances J Crosby;

Van Alstyne, 1868




238 NIFANANISHWE nawe mwokozi

238

1. Nifananishwe nawe Mwokozi, ni haja yangu iliyo kuu. Ninakuomba, na kwa machozi, nikufuate, Bwana wa juu!

Pambio:
Nifananishwe nawe Mwokozi, mwenye upendo, safi halisi! Unitakase, unijalize! Nifananishwe nawe zaidi!

 

2. Nifananishwe nawe Mwokozi, mwenye rehema, pendo ajabu! Niwapeleke kwa Mkombozi walioshindwa na majaribu!

 

3. Nifananishwe nawe Bwanangu, Mtakatifu, mwenye saburi! Niwe mnyofu kazini mwangu, mtu thabiti bila jeuri!

 

4. Nifananishwe nawe Mwokozi! Nimiminie pendo moyoni! Nibadilishe, e’ Mkombozi, niwe tayari kwenda mbinguni!

Thomas O. Chisholm, 1866-1960
O , to be like thee, blessed Redeemer, R.H. 412




267. BABA nakuomba leo na mapema

267

1. Baba, nakuomba leo na mapema: Niongoze pote kwa mapito meme!

Pambio:
Baba yangu, sikiliza ombi langu leo! Baba, nakusifu! Unanisikia.

2. Nistahimilipo kazi za mchana, unitie nguvu, nakuomba, Bwana!

 

3. Hata jua kuchwa liagapo njia, Baba, nakuomba: Unilinde pia!

 

4. Maadui wengi watuwindawinda, kwa maisha yetu Mungu ni mlinda.

 

5. Katika utoto na ujana tena, ne uzee pia: omba, kesha, shinda!

A. Cummings




268. E’YESU ingia rohoni kabisa

268

1. E’ Yesu, ingia rohoni kabisa, uniweke huru nakunitakasa, nipate kushirikiana na wewe katika mateso na raha daima!

Pambio:
:/: E’ Bwana, nijaze upendo wa mbingu nao uthabiti, niwe mshindaji! :/:

 

2. Siombi ufalme, siombi heshima, naomba kupewa neema daima, nijue ukweli wa neno la Mungu: Mtoe miili na iwe dhabihu!

 

3. Ingia rohoni, unichungulie, na katika yote unisaidie, nipate kabisa kusudi na nia kujitoa kwako, kukutumikia!

 

4. Hakuna la huku litanizuia nisifananishwe na Yesu Masiya. Nitumainije kufika mbinguni nisiposhiriki Mwokozi mpendwa!

Emil Gustavsson, 1892
O Jesus, min Jesus,