103 SIKU kubwa ya mashangilio inatufikia tena




104 LO! horini Bethlehemu




105 WAKATI wa noeli nafika kwenye hori




106 TUIMBE asubuyi iyi juu yasiku manabii Walioitabiri




253 SIKU ya furaha inatufikia

253

1. Siku ya furaha inatufikia, siku nzuri katika nchi. Mungu asifiwa mbali na karibu! Malaika wanamshukuru Bwana.

 

2. Huko Bethlehemu alipozaliwa Yesu Kristo Mwokozi wetu, pendo la Mwenyezi likadhihirika; raha ya mbinguni imefika kwetu!

 

3. Ni karama kubwa tuliyoipewa kwa mkono wa Baba Mungu. Roho mfariji anatuongoza, atuonya njia iendayo kwake.

J.D. Falk, 1816
Sweet the moments, rich in blessing, R.S. 566; R.H. 701




254 E’ROHO yangu

254

1. E’ roho yangu, sikiliza vema, wimbo wa juu unatufikia! Shangwe na raha unatuletea, amezaliwa Mkombozi wetu.

Pambio:
Ahimidiwe Mungu wa mbingu! Na duniani iwe raha na amani!

 

2.Ninafurahi kwani wimbo huo tungali tunausikia huku. Na kwa upendo Mungu aita: “Mfike kwangu, nitawapa raha!”

 

3. Katika nchi, mbali na karibu, sauti ya Mwokozi inavuma. Watu wa dhambi wanakuja kwake, awapokea na awaokoa.

F.W. Fabe




255 ZIMETIMIZWA Ahadi njema

255

1. Zimetimizwa ahadi njema: Amezaliwa Mwokozi wetu! Na yote Mungu aliyosema kwa manabii kwa ajili yetu, tumeyapata na kuyaona katika Yesu, mwanawe Mungu. Alitujia na tumepona, twaweza wote kufika mbingu.

 

2. Alijidhili kuwa maskini, na alifika ulimwenguni, Mwokozi wetu, twaiamini. Walimlaza katika hori. Na utukufu kwa Baba yake aliuacha, rehema kuu! Na twende sote horini kwake, tumsujudu aliye juu!

 

3. Mtoto huyo – mfano wetu, si mtu tu, bali Mungu pia. Akawa mwenye kutukomboa, kwa Golgotha alitufilia. Tulipotea vibaya sana katika dhambi na ukaidi, kwa umaskini wa Yesu Bwana twapata kuwa wote tajiri.




256 ASUBUHI na mapema

256

1. Asubuhi na mapema siku ya habari njema twende sote Bethlehemu! Mungu ameturehemu!

 

2.Nyota kubwa inang’aa ju’ ya nyumba ana’kaa Mwana wake wa pekee. Mbele yake tujiweke!

 

3. Wachungaji wasikia nyimbo zao malaika: ” Asifiwe Mungu juu, duniani raha kuu!”

 

4. Mariamu anachoka, safarini wana’toka, analaza mwana ndani ya sanduku la majani.

 

5. Wachungaji wanafika, na magoti wana’piga; waliacha kundi lote kushukuru Yesu wote.

 

6. Mwana yule ni Mwokozi, msaada, Mkombozi. Neno la kuaminiwa, Mungu ametushukia!