93 SIKU chache

93

1. Siku chache, na tena wakristo watakwenda kumwona Mwokozi, siku chache na wataipewa thawabu na taji ya uzima.

Pambio:
Nangoja sana Bwana Yesu kama zamu angojavyo asubuhi. :/: Kwa dalili zote ninaona sasa kwamba Yesu yu karibu ya kurudi:/:

 

2. Siku chache za vita ya huku, tena Yesu Mfalme atakuja; tutaona furaha na raha, atatupeleka kwake juu.

 

3. Siku chache machozi ya shida, Mungu atayafuta kabisa. Na baada ya siku si nyingi kwa lango nitaingia mbingu.

 

4. Baragumu la mwisho ‘talia, waminifu watachukuliwa; wote wataingia mbinguni kukaa pamoja na Mwokozi.

J.F. Thori

[youtube https://www.youtube.com/watch?v=qByPCSUaE-o?feature=oembed&w=500&h=281]




94 LO! nuru inapambazuka

94

1. Lo! Nuru inapambazuka, na vivuli vya usiku vyakimbia; unaulizwa: U tayari? Yesu yuaja upesi!

Pambio:
Na kama vile ‘pepo uvumavyo po pote, habari iendavyo ulimwenguni mwote. Ni neno la furaha, matumaini yetu: Yesu yuaja upesi!

 

2. Vizazi vingi vimefungwa utumwani kwa minyororo migumu; uhuru ni kwa Bwana Yesu, naye yuaja upesi!

 

3.Na watu wengi waamka, nuru ya injili yafukuza giza. Tutatwaliwa ‘ju mbinguni; Yesu yuaja upesi!

C” Hyllestad, 1895




95 NCHI nzuri yatungoja

95

1. Nchi nzuri yatungoja huko juu ya mawingu, watakapokusanyika wateule. Siku zina’tubakia zinapita mbio sana; waminifu watarithi nchi nzuri.

Pambio:
:/: Lo! Ufalme wake Mungu u karibu!:/: Uwe safi, roho yangu, ukakeshe siku zote! Lo! Mfalme wake Yesu yu karibu!

 

2. Twaamini tutaona nchi ile kwa uwazi, tunangoja sana Mkombozi wetu; kwa dalili tunaona siku yake ni karibu; zinatuarifu Yesu aja hima.

 

3. Maandiko yanasema: Mkombozi atakuja, katika mawingu ataonekana. Haleluya! Haleluya! Atafunga yule mwovu, aliyejaribu kutuangamiza.

 

4. Katika kungoja Yesu watu wengi wamechoka; waamshe, uwaonye kwa dalili! Kwani neno lake Mungu latimizwa mbio sana, tunaona kwamba yesu yu karibu.

D.W. Whittle




98 SIKU moja tutaona Utukufu wake Yesu

98

1. Siku moja tutaona utukufu wake Yesu, kama nuru ya umeme atakavyoonekana.

Pambio:
Uhubiri neno lake, kwa bidi’ mahali pote! Siku ni karibu sana; Bwana Yesu atakuja.

 

2. Tangu kale tumengoja siku ya uhuru wetu. Hata nguvu ya mauti itaisha siku ile.

 

3.Heri gani ya wakristo kumlaki Bwana yesu! Watavikwa nguo safi huko juu kwa Mwokozi.

 

4. Pasha hi’habari njema, na wagonjwa uwaponye! Uokowe wapotevu! Wende mbio, usikawie!

 

5. Kwa dalili tunaona kwamba Yesu yu karibu, na Mfale atakuja ‘tupeleka kwake juu.




99 SIKU moja nitamuona Bwana Yesu

99

1. Siku moja nitamwona Bwana Yesu uso wake. Na milele kwa furaha nitaka’ karibu naye.

Pambio:
Nitamtazama Yesu ju’ ya nyota zote pia, huko kwa ukamilifu nitajua nguvu yake.

 

2.Hapa ninaufahamu kwa sehemu wema wake, huko nitamtazama na kushiba kwa kuona.

 

3. Shangwe gani kwa Yesu! Shida zote zitaisha, giza haitakuwapo, na huzuni itakoma.

 

4. Yesu atafika mbio, Lo! Mwenyewe atashuka! Tutanyakuliwa juu ili kumlaki Bwana.

 

Face to face with Christ my Saviour, R.H. 781




101 E’MLINZI twauliza: ”Yesu atakuja lini?

101

1. E’ mlinzi, twauliza: Yesu atakuja lini? Asubuhi ya sayuni ni karibu? Tuambie! Msafiri, yainue macho yako, angalia! Asubuhi ni karibu, usimame, usimame!

 

2. Siku heri ya sabato ya milele ni karibu, na dalili yake Yesu hapo itaonekana. Na rohoni tunaona nchi nzuri ya ahadi. Asubuhi ni karibu, na ahadi zatimia.

 

3. Katika Yerusalemu, mji mpya wa mbinguni, Yesu atatumiliki kwa upendo na amani. Baragumu italia, nasi tutaisikia. Yesu ni karibu sana kutukaribisha kwake.

Sidney S. Brewer




257. SIKU ya kuisikia parapanda

257

1. Siku ya kuisikia parapanda yake Mungu, ikiita wateule wake wote, kwa neema tutakaribishwa na Mwokozi wetu katika kutano kubwa huko juu.

Pambio:
Tutakaribishwa kwake, tutakaribishwa kwake, tutakaribishwa kwake katika kutano kubwa huko juu.

 

2. Mungu anawafufua wafu wake siku ile, na wakristo hai watabadilika, wote watanyakuliwa kumkuta Bwana Yesu, tutakusanyika wote huko juu!

 

3. Wimbo wa mbinguni kama maji utakapovuma, utukufu wake Yesu tuta’ona. Nami pia kwa neema nitafika siku ile kusikia neno lake la “karibu!”

James M. Black, 1893
When the trumpet of the Lord shall sound, R.S. 528




290. BARAGUMU litalia sana

290

1. Baragumu litalia sana, watu wote watalisikia. Waliokufa watafufuka na wazima watabadilika.
:/: Nani anayeweza? Yesu, mweza yote. :/:

 

2. Na wenye uwezo wa dunia watatetemeka siku ile, na hawataweza kuinuka kutazama uso kama jua.
:/: Nani anayeweza? Yesu, mweza yote. :/:

 

3. Najua Mchunga wangu mwema, anichunga kwa maisha yangu. Na siku ya mwisho nikishinda, sitaona uchungu wa kufa.
:/:Nani Mchunga mwema? Yesu, mweza yote. :/:

 

4. Mbinguni hakitafika kitu cha uchafu, dhambi na kuasi. Wasiomwamini Bwana Yesu, gadhabu ya Mungu yawangoja.
:/: Nani atahukumu? Yesu, mweza yote. :/:

 

5. Mimi Yesu mzabibu kweli, Baba Mungu ndiye mkulima, na ninyi matawi ndani yangu, na hamwezi neno bila mimi.
:/: Nani ni mzabibu? Yesu, mweza yote. :/:

 

6. Unayempenda Baba Mungu, lazima upende ndugu yako; ukiwa hupendi ndugu yako, huwezi kupenda Baba Mungu.
:/:Nani aliyesema? Yesu, mweza yote. :/:

 

7. Nawapenda, mwisho wa upendo, na ninyi mpate kupendana; hivyo mataifa wataona ya kwamba m watu wangu kweli.
:/: Nani mwenye upendo? Yesu, mweza yote. :/:

 

8. Sisi watumishi wake Mungu, tumeacha vyote vya dunia. Tumemchagua Bwana Yesu, tuwekwe kuume kwake Mungu.
:/: Tumshukuru nani? Yesu mweza yote. :/:

THAMBI Aae

[youtube https://www.youtube.com/watch?v=iC4iaUPKt78?feature=oembed&w=500&h=375]