30 TARUMBETA lake Kristo linalia pande zote

30

1. Tarumbeta lake Kristo linalia pande zote, na wakristo wote wanajipanga vita ju’ ya mahodari wa shetani. Kweli tutashinda, kwani Yesu yupo mbele.

Pambio:
Twende, Yesu a’tuita, twende na wakristo wote! Twende, na tusiogope, Yesu yupo mbele yetu!

 

2. Neno la akida wetu lipo: «Mniaminie»! Naye anatangulia, tunakuja wote mbio. Kwa silaha zake Mungu kila mtu atashinda, kwani Yesu yupo mbele.

 

3.Na tukiwa mbali ya akida wetu tutashindwa, tutafungwa na adui na pengine kupotea. Walakini kule mbele watu wote watashinda, kwani Yesu yupo mbele.

 

4. Tarumbeta litalia tena, vita itakwisha, na askari watapata raha na matunzo. Watapumzika na milele watashangilia, kwani Yesu yupo mbele




74 MGENI mimi hapa mahali pa ugeni

74

1. Mgeni mimi mahali pa ugeni, na kwenda mbali mno katika nchi nzuri. Na ni mjumbe huku kutoka Mungu wetu, nina habari ya Mfalme.

Pambio:
Habari yake nzuri sana, furaha yao malaika: «Mpatanishwe sasa na Mungu Baba yetu»! Habari yake ndio hiyo.

 

2. Salamu ya Mwokozi kwa kila mtu hapa: Urudi kwake Mungu, utoke utumwani! Ufike kwake Yesu, tubia dhambi zako! Habari hiyo ya Mfalme!

 

3. Mbinguni nchi nzuri, yapita vitu vyote, furaha huko tele na raha ya milele. Ukiamini Yesu uta’pokea huko. Habari hiyo ya Mfalme!

E.T. Cassel
I am a stronger here, R.S. 75




114 IMBA habari njema: Mungu apenda wote

114

1. Imba habari njema: Mungu apenda wote! Uihubiri damu ituponyayo roho! Taja karama kubwa: Mwana alitujia, pasha habari hiyo kwa kila mtu!

Pambio:
Yesu msalabani alifilia wote, alitupatanisha na Mungu, Baba yetu. Pazia la hekalu likapasuka huko, njia imefunguka kwa wewe, nami!

 

2.Uwaimbie wenye shida na sikitiko na wapigao vita katika majaribu! Imba katika miji, pasha habari njema: Yesu awatafuta kwa pendo kubwa!

 

3.Imba katika giza, lisipofika jua, uwaimbie wote, watu wa kila bali! Imba mapema sana, na adhuhuri pia, sifu Mwokozi hata usiku waja!

Elsa Eklund, 1918?




174 PENDO kubwa la Babangu linang’aa siku zote

 174

1. Pendo kubwa la babangu linag’aa sikuzote, walakini anataka sisi tuwe nuru huku!

Pambio:
Nuru yetu iangae mbele ya wenzetu huku, hata mtu ‘moja moja aione njia njema!

 

2.Dhambi zimetia giza huku chini duniani, walakini watu wengi wanatazamia nuru.

 

3.Ndugu yangu, angalia, taa yako iwe safi! Na kwa nuru waokoe wenzi waliopotea!

P.P. Bliss
Brightly beams our Father’s mercy, R.S. 455




175 SHAMBA la Mungu limeiva

175

1. Shamba la Mungu limeiva, litayari sasa kuvunwa. Wavunaji mfike mbio kuyavuna mavuno yake!

Pambio:
Bwana Yesu, twakuomba, uwatume watenda kazi wakusanye miganda yote kwako Yesu, Mwokozi mwema!

 

2.Uwatume mapema sana, na wengine kati’ mchana, hata saa ya magharibi uwaite wavuni wako!

 

3. E’mkristo anakuita, wende mbio, usichelewe! Macho yako uyainue kwani Yesu aja upesi!

J.O. Thompson, 1894




176 MUNGU akutaka kati’ shamba lake

176

1. Mungu akutaka kati’ shamba lake, nenda na wengine kumtumikia! Ujitowe kweli kwake Mungu wetu! Uhubiri neno lake pande zote!

 

2. Ukumbuke Yesu, jinsi apendavyo! Anawatafuta waliopotea. Uwapende nawe kwa upendo wake, naye atakupa nguvu na baraka!

 

3. Uliyemwamini nenda mbio sana kati’ shamba lake, usingoje bure! Utumike vema, omba kwa bidii, na thawabu yako utaipokea!

F.R. Engelke




178 YESU kutoka mbinguni aliingia huku nchi

178

1. Yesu kutoka mbinguni aliingia huku chini ya giza na dhambi, ili atuokoe.

Pambio:
Nenda, nenda! Fanya mapenzi ya Yesu! Omba kupata sehemu kati’ ya mavuno makubwa!

 

2. Wanapotea gizani wengi wa ndugu zako. Nenda kapashe habari: “Leo wokovu uko”!

 

3.Nenda kawaubirie watu wa mataifa neno la Yesu Mwokozi! Anakuita leo.

Paul Rader




180 BWANA Yesu anatuuliza: ”Nimtume nani mavunoni?”

180

1. Bwana Yesu anatuuliza: “Nimtume nani mavunoni? Watu wenye dhambi wapotea, watolee Neno la neema! ”

Pambio:
“Mungu wangu, sema nami! Uniguze sasa kwa makaa! Mungu wangu, sema nami! Mimi hapa, unitume sasa!”

 

2. Mtumishi wake Bwana Mungu alisema: “Mimi sistahili”. Aliposikia moto safi, akasema: “Unitume mimi”!

 

3. Mataifa mengi wanakufa, hawajui Yesu na wokovu.Twende kwao mbio, tuhubiri neno la wokovu wake Yesu!

 

4. Siku za mavuno zitapita, watumishi watarudi kwao. Bwana wao atawapokea na kusema: “Ulifanya vema”!

Hear the Lord of harvest, R.H. 559


[youtube https://www.youtube.com/watch?v=R8SIyCf45go?feature=oembed&w=500&h=281]




182 KISA cha kale nipe

 182

1. Kisa cha kale nipe, habari ya mbinguni, ya Bwana Mtukufu, ya pendo lake Yesu! Niambie neno lake, nipate kusikia, mnyonge mimi huku, mjinga, mkosaji. Kisa cha kale nipe, kisa cha kale nipe, kisa cha kale nipe, cha pendo lake Yesu!

 

2. Sema kwa taratibu nipate kuelewa habari ya wokovu na damu ya Mwokozi! Simulia mara nyingi, nisije kasahau, niikumbuke tena maisha yangu yote!

 

3. Taja habari hiyo kwa wema na kwa pendo, Mwokozi alikufa kutukomboa sote. Na ikiwa unataka kunifariji mimi, nisimulie ile habari ya zamani!

 

4.Nipe habari hiyo ikiwa waniona ninaipendelea fahari ya dunia! Siku nitakapo kufa ‘tapenda kusikia habari ya zamani: Mponyi mwema Yesu.

W.H. Doane
Tell me the old, old story, R.S. 132; R.H. 294




183 PANDA mbegu njema

 183

1. Panda mbegu njema, anza asubuhi, na uwaokoe watu wa shetani! Kwa wakati wake vuno litaivya, chumo utapata kwa furaha kuu.

Pambio:
:/: Twende tukavune, twende tukavune, kwa furaha kubwa twende tukavune! :/:

 

2. Panda mbegu njema juu ya milima! Na tuendelee hata mabondeni! Neno lake Mungu litawafungua watu wa gizani, kwa furaha kuu.

 

3. Panda mbegu njema hata kwa machozi, ukumbuke Yesu, leo uhubiri! Bwana wetu, Yesu, atakuja tena na thawabu yetu kwa furaha kuu.

A.M. Simpson
Sowing in the morning, R.S. 463




184 NITAKWENDA mahali pa giza

184

1. Nitakwenda mahali pa giza na dhambi kuhubiri Injili ya nuru, ili watu wasiosikia habari wafahamu upendo wa Yesu.

Pambio:
Nitakwenda mahali pa giza na dhambi, hata wote wapate kuona wokovu.

 

2. Akitaka niende kwa watu wagumu na kuacha rafiki na ndugu, hata wakinitaja: ” ‘pumbavu ” na “bure”, nachagua mapenzi ya Yesu.

 

3.Uliyezipoteza dakika na saa kwa tamaa ya mambo ya huku, uamke na uwaokoe wenzako, hata wasipotee kwa dhambi!

 

4. Watu wengi wangali watumwa gizani, wanangoja kupata uhuru, Yesu ananituma, niende upesi kuhubiri maneno ya nuru.

Margeret M. Simpson




185 NEHEMA kubwa ya Mungu wetu

185

1. Neema kubwa ya Mungu wetu: Alikutuma kwa kazi yake kwenda kuzipanda mbegu njema katika roho za wenzako!

Pambio:
Nenda, E’ mvunaji, nenda, e’mvunaji! Nenda kapande mbegu njema, nenda, e’mvunaji!

 

2. Njia ikionekana ndefu, neno la Mungu ni aminifu: “Kwa macho yangu nakuongoza, jangwani nitafanya njia”.

 

3. Ikiwa ndugu hawakuoni, mtumikie Mwokozi vema! Bwana anayetazama wewe, anampenda mwaminifu.

 

4. Hata ukiwa mdogo sana, nenda upesi shambani mwake, labda utaliokota suke lililoachwa na wenzako.

 

5. Neno na nyimbo hazitatosha kuwaamsha wafanya dhambi, bali mwenendo ulio safi utawavuta ndugu zako.

 

6. Na usichoke kupanda mbegu katika pendo na tumaini! Ukizipanda kwa shida nyingi, kwa shangwe kubwa utavuna!

 

7. Siku za kazi zita’pokwisha tutahamia mbinguni juu; tutawaona wenzetu wote tuliovuta kwa Mwokozi.

Eric Bergqvist 1898




186 FANYIA Mungu kazi

186

1. Fanyia Mungu kazi, mbio usiku waja! Mtumikie Mungu siku zako zote! Anza mapema sana, dumu mchana kutwa! Mbio usiku waja, kazi itakwisha.

 

2. Fanyia Mungu kazi kama kungali jua, usipoteze bure siku zako huku! Uyatimize yote bila kukosa neno! Mbio usiku waja, kazi itakwisha.

 

3. Fanyia Mungu kazi, saa yapita mbio! Fanya bidii sana kuokoa ndugu! Mtumikie Mungu kwa nguvu yako yote! Mbio usiku waja, kazi itakwisha.

 

T. Annie L. Coghill, 1854 M. Lowell Mason, 1864
Work for the night is coming, R.S. 429

[youtube https://www.youtube.com/watch?v=Hc9BgKGWv8o?feature=oembed&w=500&h=281]




187 TUWAVUNAJI wake Mungu

 187

1. Tu wavunaji wake Mungu, kwa neno lake tunakwenda kuvuna ngano zake Yesu alizojinunulia. Kwa shangwe tunaliingiza ghalani mwake vuno lake. Tunamsifu Yesu aliyekomboa vuno lake.

Pambio:
Twende kati’ shamba lake, Bwana a’tuita! Vuno linaivya sana, usikie mwito! Siku zetu za mavuno zinatupitia mbio. Siku zetu, siku zetu zinabaki chache.

 

2. Tu wavunaji, twende sasa tukalivune vuno lake, na kwa bidii na imani tukusanye ngano ghali! Katika pendo kubwa mno anawataka wote, Yesu, na tukiacha suke dogo ataona mara moja.

 

3. Wakati wetu ni mfupi, a’ita tena, twende mbio! Atujalize uhodari, nguvu ya kuvumilia! Usichelewe bure sasa, watenda kazi ni wachache! E’mvunaji wake Yesu, utumike kwa bidii!




209 UWATAFUTE wanao potea

209

1. Uwatafute wanaopotea, na kwa upendo watoe dhambi! Lia pamoja na wenye huzuni, uwapeleke kwa Yesu Mwokozi! Uwatafute wanaopotea! Yesu Mwokozi awahurumia.

 

2. Anatafuta waliokimbia, anawangoja warudi upesi. Uwafundishe kwa pendo na kweli ju’ ya neema na haki ya Yesu!

 

3.Ndani ya roho na katika siri labda waona shauku ya Mungu. Uwaongoze kwa Yesu Mwokozi, wafahamishe upendo wa Mungu!

 

4.Uwatafute wanaopotea! Mungu atoa upendo na nguvu. Uwapeleke kwa Yesu mpozi, Mwenye huruma na afya kwa wote!

Fanny Crosby, 1869
Rescue the perishing, R.S. 345; R.H. 561 




210 IMBA injili ya Yesu kwa moyo na roho kabisa

210

1. Imba injili ya Yesu kwa moyo na roho kabisa! Lango la neema yake ni wazi kwa watu wote.

Pambio:
Imba, imba injili, na watu wasikilize! Imba injili ya Yesu, maneno ya pendo lake!

 

2. Imba injili ya Yesu! Yaleta uhuru kwa wote. Imba habari ya damu inayotakasa moyo!

 

3. Imba injili ya Yesu, kwa wimbo utawafundisha! Imba habari ya Yesu! Aweza kuwaokoa.

 

4. Imba injili ya Yesu, na raha na matumaini! Imba habari ya haki, wapate kujua Mungu!

 

5. Imba injili ya Yesu, hubiri amani kwa wote! Na tumsifu Mwokozi afanyaye yote vema!

Philip Philips, 1877




244 SAFARI yangu huku ikiwa hatarini

244

1. Safari yangu huku ikiwa hatarini, na ikipita katika giza na jaribu, najua kwa hakika: Mwokozi yu karibu, ninamfuata mahali po pote.

Pambio:
Nikiwa pamoja na Yesu sina hofu. Anipa furaha na heri rohoni mahali pote. Ikiwa nitayashiriki mateso yake, nitamfuata Mwokozi hata mwisho.  

 

2. Nikitangaza neno la Mungu duniani katika mataifa walio wakaidi. Nina furaha kubwa moyoni mwangu, kwani Mwokozi yu nami mahali po pote.

 

3. Na Bwana akitaka nibaki hapa kwangu, wengine wakitumwa mahali pa ugeni, kusudi langu moja: nidumu mwaminifu, na nimfuate mahali po pote!

 

4. Si lazima nijue makusudio yote, ni kazi yangu huku kumfuate yeye. Ikiwa nitabaki, ikiwa nitakwenda, nitamfuata Mwokozi po pote.

C. Austin Miller
It may be in the valley, R.H. 465




269. KATIKA bonde na milima

269

1. Katika bonde na milima, kwa mataifa mahali pote, peleka neno la wokovu! Msifu Yesu sana!

Pambio
Msifu Bwana, msifu Bwana! Na tangazeni neno lake, ‘sifuni Yesu daima!

 

2. Mapema na jioni pia hubiri neno la Bwana Yesu! Tangaza njia ya wokovu, msifu Yesu sana!

 

3. Lo! Paradiso malaika wanahimidi Mwokozi wetu. Tuimbe nasi sifa yake, tu’sifu yesu sana!

 

4.Usiyeona kufa bado, uipokee neema leo! Ujisafishe kati’ damu, msifu Yesu Kristo!

H.W. Clark




270. SIMAMA fanya vita pamoja na Mfalme

270

1. Simama, fanya vita pamoja na Mfalme! Bendera tuishike iliyo ya Mwokozi! Mwenyezi huongoza majeshi yake huku. Adui wote pia washindwa mbele yake.

 

2. Sikia baragumu, linatuita sasa! Tuendelee mbele, kusudi ni kushinda! Tusiogope kamwe hatari ya shindano, pigana na adui kwa nguvu yake Mungu!

 

3. Sima, fanya vita kwa jina lake Yesu! Hatuna nguvu sisi, tunamtegemea. Na kwanza tuzivae silaha zake Mungu! Tukeshe siku zote, tuombe kwa bidii!

 

4. Shindano letu hapa ‘takwisha siku moja; twapiga vita leo, baada pumziko. Na kila mshindaji atapokea taji, na utukufu tele karibu na Mfalme.

Georg Duffield, 1858




271 UWATAFUTE wenzako wapoteao mbali

271

1. Uwatafute wenzako wapoteao mbali! Yesu mwenyewe apenda kuwaokoa wote.

Pambio
Uwatafute wenzako wapoteao mbali! Pasha habari ya Yesu na ya wokovu wake!

 

2.Uwatafute wenzako kwa neno la upendo! Mungu atalibariki na kulithibitisha.

 

3.Uwatafute wenzako kwa’jili ya Mwokozi! Aliwakomboa wote, ni mali yake kweli.

 

4.Uwatafute wenzako kabla ajapo Yesu! Wasipotee kabisa, uwaokoe mbio!

Fred P. Morris




272. NANI ni wa Yesu

271

1. Nani ni wa Yesu? Amtumikie! Atafute watu na kuwahubiri! Nani anataka kujitoa leo, kufuata Yesu katika mateso?

Pambio
Nani ni wa Yesu? Amtumikie! Nani atakaye na amwitikie! Mimi ni wa Yesu, nimtumikie, nitafute watu, kwake warudie!

 

2. Kwa upendo wake tunalazimishwa kutafuta wenye dhambi na makosa. Tunaendelea kuwavuta kwake, hata wanaomba: Mungu tuokoe!

 

3. Yesu alitununua sisi sote ju’ ya msalaba na kwa damu yake. Kwake tumepata raha na uhuru; tunataka sasa kuwa waaminifu!

 

4. Hata vita ikiongezeka huku tunayo bendera ya kushinda kwetu. Siku ya hatima inakaribia, itaibadili vita iwe shangwe.

Frances R. Hauergal