4 USIKU kabla yakuteswa

1. Kabla ya kuteswa, Yesu Alikusanya wanafunzi wake; Alifahamu kwamba saa yake ya kutolewa ilikaribia.

 

2. Kwa roho aliona gethesemane, Meteso yake na huzuni nyingi;  Zaidi alihofu saa ile, ata’poachwa hata naye Mungu.

 

3. Alitamani saa ya pasaka pamoja na wapendwa wake huku. Katika pendo lake kubwa sana Aliyashinda majaribu yote.

 

4. Akautwa’ mkate, aka’mega, Twaeni, mle, hu’ ni mwili wangu!  Na akawapa wanafunzi wake. Wa heri kila mtu aminiye.

 

5. Ba’daye akawapa na kikombe, Na akasema: Nyweni nyote hiki! Ni damu yangu inayomwagika kwa ondoleo la makosa yote.


[youtube https://www.youtube.com/watch?v=xaJOREk2_oY?feature=oembed&w=500&h=281]




43 JUU ya mwamba umejenga kanisa lako duniani

43

1. Juu ya mwamba umejenga kanisa lako duniani, umeliweka huru kweli katika damu yako, Yesu.

Pambio:
Juu ya mwamba, juu ya mwamba huru na safi umelijenga. Juu ya mwamba, juu ya mwamba, huru na safi tusimame!

 

2. Neema kubwa! Nimepata sehemu yangu kanisani. Vita ya roho imekwisha, umenijaza utulivu.

 

3. Kati’ hekalu lake Mungu nimefanyika jiwe hai. Ninashiriki mwili wake kama kiungo chake Kristo.

 

4. Ju’ ya msingi huo safi liwe kanisa lako zima! Vyote vikiondoka huku, litasimama, litashinda.

Charles P. Jones, Otto Witt, 1922




60 NIHERI kuona ndugu njiani pa kwenda mbinguni

60

1. Ni heri kuonga ndugu njiani pa kwenda mbingu. Tukinyong’onyea sana kwa kuwa tu peke yetu, kushirikiana kwa ndugu kunaturudisha moyo, na Mungu atupa nguvu tukiyainua macho.

 

2. Twafungamana rohoni, tulio wa nyumba yake, huoni ulimwenguni kushirikiana kwetu. Na tuna Mwokokozi mmoja, imani ni moja pia, watoto wa baba ‘moja twashika sheria yake.

 

3. Furaha ya ulimwengu haitatuvuta tena, Twaona kung’aa kwake ni bure na bila kisa. Lakini tukikusanyika kwa jina la Mungu Baba, atuandalia kweli karamu ilio bora.

 

4. Tukivumilia hata ukomo wa mashindano, mbinguni tutawaona wakristo wapenzi wote. Hatutatawanyika huko, tu wote umoja kweli, milele tuta’pokaa nyumbani kwa Baba yetu.

Kirsten D. Hansen Aagaard, 1870




61 ENYI wetu wa Sayuni

61

1. Enyi watu wa Sayuni, kundi dogo la Mwokozi, Yesu aliwanunua kuwa mali yake Mungu. Sasa mnapita njia ya miiba na hatari kati’ nchi ya ugeni; bali mbingu mtafika.

 

2. Kumwamini, kumpenda Yesu ni uheri wetu; amri zote zinashikwa kwa upendo na amani. Kwa imani twaokoka, pendo ni uzima wetu. Yesu utusaidie, utujaze pendo lako!

 

3.Juu ya msingi huo, Yesu, unijenge mimi, na zaidi niungane nawe na kanisa lako! Sisi tu matawi yako, tushirikiane sana, na katika kundi nzima iwe nia moja kweli!

A.C. Rutström




172 SISI tu viungo vya mwili’ moja

172

1. Sisi tu viungo vya mwili ‘moja, tunasaidiana. Utumishi wetu tunaupenda na twasaidiana. Twasaidiana sote, twasaidiana sote. Twamaliza kwa shangilio na kwa bidii kazi yetu.

 

2. Twafurahi kwa utumishi, hata tukiwa peke yetu; walakini heri zaidi kama tukisaidiana. 3.Ikiwezekana kwa mchwa ‘dogo kujenga kisuguu, sisi nasi kwa nguvu yake Mungu tutamaliza kazi.

 

4.Na umoja wetu ni wa thamani, unapendeza Mungu; anatubariki kwa neema, anatupa tunu kubwa.

 

5. Twakuomba, Bwana, ‘tuunganishe, tujaze pendo lako! Na kwa Roho yako utubatize, tuhudumie wewe!

A.L. Skoog, 1856-1935




200 NJONI wote

200

1. Njoni wote, mle, mnywe, Yesu anasema hivyo. “Nimetoa mwili wangu kwa ajili yenu ninyi.” Kila mtu mwenye njaa aje na apate kula! Na aliye na makosa atasamehewa yote.

 

2.Ninakuja kwako, Yesu, unithibitishe moyo! Uliona umaskini, niwe mwenye uta-jiri. Nishibishe mema yako na karama takatifu! Unijaze Roho yako kama ulivyoahidi!

 

3. Yesu, ninakuja kwako niungane nawe, Bwana! Mimi mwenye udhaifu, nakutegemea wewe. Na kwa damu yako, Yesu, ninatakasika sasa. Nashiriki mwili wako katika agano jipya.

Tune: Who can cheer the heart like jesus, R.H. 518; MA. 490




279. UPENDO wake Mungu unatuunganisha

279

1. Upendo wake Mungu unatuunganisha. ‘Shirika wa watakatifu – uheri wa mbinguni.

 

2. Katika sala zetu twakaribia Baba kwa tumaini, ujasiri na kwa imani moja.

 

3.Upendo wa kikristo ha’vunji urafiki. Twalia naye kwa uchungu, furaha twa’shiriki.

 

4. Tunaachana huku kwa sikitiko sana. Kwa shangwe tena kwake Mungu twaweza kuonana.

Fohn Faweet
Blessed be the tie that binds, R.S. 946; R.H. 713