2 KIJITO kiko chenye damu itokayo Mwokozi

1.  Kijito kiko chenye damu Itokayo Mwokozi, Kiwaoshacho wakosao
    :|: Na dhambi na uchafu :|:

2. Msalabani mnyang’anyi Alikiona hima. Mnyonge mimi kama yeye
    :|: Nitakasike pia! :|:

3. Mwokozi wetu, damu yako Daima ina nguvu ya kuokoa wenye dhambi
    :|: Wa makabila yote :|:

4. Kijito hicho cha ajabu Ni tumaini langu upendo wako nausifu,
    :|: Nasifu hata kufa. :|:

5. Nimeamini, naamini Uliyenifilia, Msalabani umetoa
    :|: Maisha yako, Yesu. :|:


 

 




5 DHAHABU na feza haziniokoi

1. Dhahabu na fedha haziniokoi, Hazina na mali haziponyi roho,
Lakini kwa damu ya Yesu mwokozi nimenunuliwa nipate uhuru.

Refrain :
Nimekombozwa pasipo mali, kwa neema nimeokoka !
Ni bei ghali : kwa damu yake Alilipa deni langu.

 

2. Dhahabu na fedha hazinilipii madeni makubwa ninayo kwa Mungu.
Mwokozi alinikomboa kwa damu nipate wokovu, nitoke dhambini

 

3. Dhahabu na fedha haziufungui Mlango wa ku’karibia mwenyezi,
Lakini kwa damu nimeifikia Neema ya Mungu aliya mkuu.

 

4. Dhahabu na fedha hazinifikishi nyumbani mwa Mungu niliyemwasia,
Lakini nimekombolewa kwa damu, kwa hiyo nitachukuliwa mbinguni.


 

 




8 YESU KRISTO asifiwe!

 1. Yesu Kristo asifiwe! Alizichukua dhambi,
Ne’ma inatoka kwake kati’ damu.
Umeosha moyo wako, umekuwa safi,
huru umeondolewa dhambi kati’ damu?

Refrain:
:|: Kati’ damu :|: Umeosha moyo wako, umekuwa safi, huru?
:|: kati’ damu :|: Umcondolewa dhambi kati’ damu?

 

2. Ukilia, ukijuta dhambi hazitoki kamwe;
Haki kweli uta’pata kati’ damu.
Mambo yakusumbuayo Yesu a’ondoa mara,
Unapata ukombozi kati’ damu.

 

3. Yesu atatuchukua arusini mwake huko.
Umevikwa nguo safi kati’ damu?
Je, wajenga ju’ ya mwamba, moyo wako u mzima,
unashinda kila saa kati’ damu?

 

4. Bwana Yesu asifiwe! Aliloa damu yake,
na kwa damu ya thamani tutashinda.
Asubuhi kubwa ile vita itakapokwisha,
tutaimba kwa Furaha ju’ ya damu.

 




10 DAMU yako yenye baraka inayotuosha makosa

1. Damu yako yenye baraka Inayotuosha makosa.  

Ilitoka musalabani, Bwana YESU, alipokufa alipokufa.  

Nastahili pata hukumu, Na siwezi mimi kujiosha.  

Unioshe katika damu nipate kuwa safi kabisa!

Refrain:
Safi, Safi kweli, Safi, safi kweli!
Unioshe katika damu nipate kuwa safi kabisa!

 

2. YESU ulivikwa miiba, kuangikwa juu ya mti.  

Ulivumilia mateso, Maumivu na majeraha.  

Ninataka kijito hicho N’ende na nikasafishwe sana!  

Unioshe katika damu, Nipate kuwa safi kabisa.

 

mimi mwenye dhambi rohoni nitaona wapi mwokozi?

yesu kwako msalabani naja ninakuamini sasa.

unioshe katika damu nipate kuwa safi kabisa.

 

4. BWANA, nimefika karibu, unilinde kwako,

mille! ufungue kila kikamba, unijaze moyo mwenyewe!

na karibu ya msalaba nitakaa hata kufa kwangu.

unioshe katika damu nipate kuwa safi kabisa.


 




12 KWA badala yangu kweli Yesu alitoa damu

1. KWA badala yangu kweli Yesu alitowa damu.
Mimi huru na ni heri, Bwana Yesu asifiwe!

Refrain:
Yesu alinikomboa, lakini Si kwa dhahabu na mali ya dunia; bali damu ya mwokozi ni malipo kwa ajili yangu, Haleluya!

 

2. Tuinue msalaba, hata wote wataona Mwana wake Mungu,
hapo Alitowa damu yake!

 

3. Dunia kubwa, Yesu kristo! wingi sana wa upendo:
Yesu aliacha mbingu, alitufiliya sote.

 

4. Sitaweza kufahamu Bei ya wokovu wangu, Bali ninajuwa:
Yesu alinikomboa.




13 NANI aweza kuniweka huru?

1. NANI aweza kuniweka huru? ni Yesu mwokozi, Yesu mwokozi!
nguvu kushinda nipate kwa nani? kwa damu ya Yesu mwokozi!

Refrain:
Kuna nguvu, nguvu za ajabu kuu kati damu yake ya mwokozi! Kuna nguvu, nguvu za ajabu kuu kati damu yake Yesu.

 

2. Nitawezaje kuvunja taa? Kwa damu ya Yesu, damu ya Yesu!
Nikaribie kisima cha hai, kisima cha damu ye Yesu.

 

3. Nitawezaje kuoshwa moyoni? Kwa damu ya Yesu, damu ya Yesu!
Nitakasike katika kisima, kisima cha damu!

 

4. Nitawezaje kutenda vizuri? Kwa nguvu za damu ya Yesu, nguvu ya Yesu!
Nitawezaje kufika mbinguni? Kwa nguvu ya damu ye Yesu.


[youtube https://www.youtube.com/watch?v=cjnuogOvWSI?feature=oembed&w=500&h=281]




112 ULINDE roho na nafsi yangu chini ya damu

 112

1. Ulinde roho na nafsi yangu chini ya damu, chini ya damu! Makosa, hofu na shaka ziwe chini ya damu yako!

Pambio:
Chini ya damu yako, Yesu, ndani ya mto huo safi, unilinde kwa siku zote, chini ya damu yako!

 

2. Makimbilio ya mwenye dhambi, chini ya damu, chini ya damu, ni ukombozi kwa watu wote, chini ya damu yako!

 

3. Nijaze nguvu na pendo lako chini ya damu, chini ya damu, nipate tena kutii wewe chini ya damu yako!

 

4. Amani kubwa moyoni mwangu chini ya damu, chini ya damu, karama zako zanipa raha, chini ya damu yako.

 

5. Nijazwe Roho Mtakatifu chini ya damu, chini ya damu, daima niwe na moyo safi, chini ya damu yako.

 

Lord, keep my soul from day to day,