323 Nakutegemea Yesu, unilinde hapa chini

1. Nakutegemea Yesu, unilinde hapa chini. Njia yangu ndefu sana wewe ndiwe kiongozi.

Pambio:
Unitie nguvu kweli majaribu na mashaka vyazunguka roho yangu. Kweli utaniwezesha.

 

2. Nilikuwa mbali nawe, hata hivyo ‘kanifia. Ulipenda roho yangu, nakupenda Bwana wangu.

 

3. Kao nzuri la mbinguni, natamani kufikako. Unitengeneze tena yainue macho yangu.

 

4. Hapa chini duniani ibilisi anguruma. Anataka kutumeza, sifa kwako twazunguka.

 

WATONGOKA Mulonge Erasto, 1968




324 Bwana Yesu atashuka mbingu na sauti za wamalaika

1. Bwana Yesu atashuka mbingu na sauti za wamalaika.

Pambio:
:/:(Lakini wewe) mwovu, ujue kama utaenda wapi. Itakuwa furaha kubwa, kwa wale wataenda na Mwokozi. :/:
:/: (Itakuwa furaha) itakuwa furaha kubwa, kwa wale wataenda na Mwokozi.:/:

 

2. :/: Waliokufa katika Bwana, wao watafufuliwa kwanza:/:

 

3. :/: Na kisha sisi tulio hai tutanyakuliwa mbinguni. :/:

 

4. :/: Nayo furaha ya wenye dhambi itageuka kuwa uchungu.:/:

 

5. :/: Nayo huzuni ya wenye haki itageuka kuwa furaha.:/:

(Mtungaji hajulikani, 1969)




325 Hapa katika dunia tunaachana mara nyingi

1. Hapa katika dunia tunaachana mara nyingi. Lakini kwa Mwokozi wetu, hatutatengwa naye.

Pambio:
Baba Mungu awe pamoja nawe. Akulinde katika njia, Uende katika amani, Tu pamoja kwa maombi.

 

2. Tukitengwa na rafiki, tunatumaini kwa Mungu, Yeye atatufariji, kwa neema na upendo.

 

3. Adui wetu watatu, mwili, dunia na shetani. Uepuke wote hawa, ngao, neno lake Bwana.

 

4. Baba Mungu twakuomba, uchunge huyumwana wako. Pamoja na jamaa lake, hata siko ya milele.

 

TAMBI Eae Munaongo, 1945




326 Siku kuu ya Mungu imekaribia

1. Siku kuu ya Mungu imekaribia, mwaliko umetumwa kwako. Mda ni mfupi, tujitayarishe, kwenda kumlaki Bwana Yesu.

Pambio:
Siku inakuja, yawaka kama moto, kimbia hukumu yake Bwana. Siku inakuja, yawaka kama moto, kimbia hukumu yake Bwana.

 

2. Wewe unasema: ni siku nyingi twaalikwa na wahubiri. Ufahamu kama siku moja kwa Bwana, ni kwama miaka elfu moja.

 

3. Rafiki ‘jiulize, je umeokoka, kwa matendo na tabia yako? Kama bado, mpendwa, hujui amani, fanya hima uokoke sasa.

MAROYI Birindwa, 1979




327 Katika giza la usiku, pakawa na kelele kuu

1. Katika giza la usiku, pakawa na kelele kuu. Tazama Bwana yu karibu, tokeni mwende kumlaki.

:/: Tazama, Bwana yu karibu, Tokeni mwende kumlaki. :/:

2. Na wanawali wote kumi, wakachukua taa zao. Lakini tano wapumbavu wapungukiwa na mafuta. 3. Wakawasihi wa busara, tupeni kwa mafuta yenu. Zinazimika taa zetu, na hatujui tutendalo.

4. Wakawajibu wa busara, hayatutoshi sisi nanyi. Mwendeni kwao wauzao mkajinunulie sasa.

5. Na wakaenda kununua, akaja Bwana wa arusi. Watano walio tayari wakaingia arusini. 

6. Mlango hapo ukafungwa, halafu wale wapumbavu wakaja nao, wakalia, tufungulie, Bwana wetu.

7. Bwana arusi akajibu: amina, siwajui ninyi. Kesheni basi, kwa sababu hamjui siku yangu.

:/: Tazama, Bwana yu karibu. Jitayarishe kumlaki.:/:

8.Gizani, nje ya arusi, wakasimama wapumbavu. Kulia wakalia sana, tufungulie, Bwana wetu.

:/: Na jibu likatoka wazi: Mmechelewa kuingia. :/:




328 Bwana Yesu ‘tuongoze, wende mbele yetu

1. Bwana Yesu ‘tuongoze, wende mbele yetu. Sisi tuwe nyuma yako, tufike Sayuni. Sisi peke hatuwezi kuongoza njia yetu. Ulisema peke yako, wewe ndiwe njia.

 

2. Huku chini duniani tunahangaishwa. Vinavyotuhangaisha vitabaki huku. Bwana Yesu tunachoka, tuwezeshe safarini. Kwa kungoja baragumu tushushie Roho.

 

3. Mambo mengi yanafichwa kwa kukosa moto. Watu wengi wanacheza na maovu yao. Wanadhani huwaoni, mwovu anawadanganya. Tuma uamsho, Bwana, urudishe wengi.

 

4. Twakwambia leo, ndugu, usidanganyike. Bwana Yesu anajua njia zako zote. Hata ikiwa usiku kwake kuna nuru wazi. Acha njia zile ndugu, saa zingaliko.

 

5.Usidhani hakuoni, anavumilia. Anangoja siku ile atimize yote. Una heri leo, ndugu, kwani tunakukumbusha. Fika leo kwa Mwokozi, saa zinapita.

 

6. Anabisha mlangoni, umfungulie, anataka aingie kuokoa wewe. Mbona humfungulie? Anakuhitaji wewe. Ne’ma kwako itakwisha, utahukumiwa.

 

7. Una heri, ndugu, wewe uliye hokoka, Bwana Yesu akirudi, tutashangilia. Tutamfanana Yesu, na kurithi mji ule, wa milele na milele, mji wa heri…

 

MUBIKWA Onesimo, 1964




300 Mungu awabarikie nyote na awe pamoja nanyi!

1. Mungu awabarikie nyote na awe pamoja nanyi! Awalinde kwa amani!

Pambio:
Mungu n’awe nanyi siku zote! Mungu n’awe nanyi daima hata mwisho wenu wa safari! Mungu n’awe nanyi daima hata tuonane huko juu!

 

2. Mungu wetu awalinde pote na kuwahifadhi vema kwa mikono ya rehema! Mungu n’awe nanyi siku zote!

 

3. Mungu awaangazie nuru, na awashibishe sana kwa fadhili zake Bwana! Mungu n’awe nanyi siku zote!

 

4. Mungu awainulie uso! Na wakati wa kuhama mpelekwe kwa salama! Mungu n’awe nanyi siku zote!

 

5. Mungu awabarikie nyote, awalinde m-we huru, awaangazie nuru! Awainulie uso wake!

J.E. Rankin / Daniel Hallberg
God be with you till we meet again, R.S. 942; R.H. 722




301 Njioni (sic) tumwimbie Bwana

1. Njioni (sic) tumwimbie Bwana tumfanyie shangwe kuu. Mwamba wa wokovu wetu, tuje kwake na shukrani, tumfanyie shangwe kuu, Bwana ni Mungu mkuu, na Mfalme wa wafalme, tena Bwana wa mabwana.

 

2. Mikononi mwake zimo bonde zote za dunia. Na vilele vya milima ndiye aliyezifanya, aliifanya bahari na nchi akaiumba, njioni (sic) wote tuabudu, tusujudu Mungu wetu.

 

3. Tupige magoti yetu mbele ya Muumba wetu. Kwani ndiye Mungu wetu nasi tupo mali yake, na kondoo zake yeye, ingekuwa heri leo, msikie neno lake msifanye mioyo gumu.

 

4. Kama huko kwa Moria siku za Munga jangwani. Hapo walinijaribu babu zenu hapo kale. Wakanipima kuona matendo yangu makuu, kwa miaka arobaini nikahuzunishwa nao.

 

5. Nikasema watu hawa waliopotoka mioyo. Hawakuzijua njia zangu niliwaonyesha, nakaapa kwa hasira yangu na kusema hivi: Wasiingie rahani mwangu ya huko Kanaani.

Yakobo Sulemani, 1971




302 Mungu wetu alituambia, tusichoke kumtumikia.

1. Mungu wetu alituambia, tusichoke kumtumikia. Wale watakaoshindwa huku watabaki huku duniani. Mungu wetu tunangoja sisi,

Mwnye enzi Yesu Mkombozi

:/: Twawekewa makao mazuri:/:
(Huku hakuna njaa)

Twawekewa makao mazuri
(Hakuna masumbuko)

Twawekewa makao mazuri
(Na hakuna kilio)

Twawekewa makao mazuri
(Wala masikitiko)

Twawekewa makao mazuri
(Na hakuna magonjwa)

Twawekewa makao mazuri
(Ni nchi ya milele)

Twawekewa makao mazuri
(Kuna fasi kwa wote)

Twawekewa makao mazuri

 

2. Bwana Mungu hakutukataa kwa dunia hii ya makosa. Watu ndio wanamkataa. Wamwamini adui shetani.

 

3. Watu watakaoshinda huku, watapata raha ya milele. Mungu alitutumia Roho, kutuonya njia yake Yesu.

Lugha Kinyanga- Masumbuko
Mfasiri: Tambi Eae Munaongo, 1967




303 Nitamwimbia Mungu na furaha, kwa sababu alishinda shetani.

1. Nitamwimbia Mungu na furaha, kwa sababu alishinda shetani. :/: Kwa furaha punda zote za Farao, walizozipanda wote wakafa. :/: :/:

Pambio:
Kule ngambo, kule ngambo wa israeli walivuka, walipomwimbia nyimbo za Musa:/: :/: Kule ngambo walivuka na furaha walipomwimbia nyimbo za Musa. :/:

 

2. Gari zote za askari kwa kupita, kwa kuwashambulia watu wa Mungu. :/: Wale wote mashujaa wa Farao, Mungu aliwafunikiza majini. :/:

 

3. Wanawake waliimba kwa furaha. Wakapiga vinubi kwatika shangwe :/: na nabii Miriamu akasema, msifuni Mungu wetu kwa furaha.:/:

 

4. Mwenyezi Mungu ni tumaini langu, tena Mungu anakuwa wimbo wangu. :/: Mwenyezi Mungu anipitia mbele, na tena ni yeye yuko ngao yangu. :/:

Wimbo wa kinyanga,
Mfasiri Tambi Eae Munaongo, 1963




304 Sifa, uwezo na heshima, kwake Yesu Mwana kondoo.

1. Sifa, uwezo na heshima, kwake Yesu Mwana kondoo. Sifa, uwezo na heshima, ni Mfalme wetu.

Pambio:
Sifa, sifa, mwimbie kwa shangwe Sifa, sifa, Mwana Kondoo.

 

2. Siku ya kuja kututwaa, tutakwenda kumlaki. Na tena tutamfanana, sifa Mwana Kondoo.

 

3.Nitafurahi kuondoka nchi hii ya mateso. Nitamkuta Bwana wangu, na Mwokozi wangu.

 

4.Ninamwimbia tu kidogo, hapa chini duniani, nitamwimbia mara nyingi, huko kwake mbingu.

Wimbo wa kifransa
Tambi aongeza maneno, 1953




305 Sifa na sifa ninakupa Yesu

1. :/: Sifa na sifa ninakupa Yesu, kweli nimwimbie Mungu :/: :/: Sifa, sifa na sifa kwa Yesu. :/:

 

2. :/: Maombi yangu Bwana yakufikie, ee! Mungu wa heri yangu.:/:

 

3. :/: Sitaki kuomba-omba kama ndege, kulia-lia porini. :/:

 

4. :/: Na sasa roho yangu inasimama. Kweli nimwimbie Mungu. :/:

 

5. :/: Na watakatifu wanasimama, wanamwimbia Mwokozi. :/:

 

6. :/: Tuna huzuni ya wandugu wetu. Wako kwa giza ya dhambi. :/:

Missionnary




306 Ninakuhitaji Mwokozi, kujazwa na Roho yako

1. Ninakuhitaji Mwokozi, kujazwa na Roho yako. Mapema, mchana, jioni, nikutumikie Yesu.

Pambio:
:/: Ninakuhitaji Yesu, nijazwe upendo wako. Na siku kwa siku, Mwokozi, nikutumikie vema. :/:

 

2. Ikiwa ni siku za kazi, ikiwa ni siku kuu. Ninakuhitaji Mwenyezi, kujazwa na Roho yako.

 

3. Nyumbani mwa baba na mama, kondeni mwa watu wengi. Popote ninapopitia, nilinde na niongoze.

 

4. Ninakuhitaji, Mwokozi, katika maombi yangu. Niombe kwa mapenzi yako, nipate yanifaayo.

 

5. Katika kitabu cha Mungu, twasoma ahadi zake. Aombaye atapewa, kwa jina la Yesu Kristo.

Missionnary




307 Walikombolewa waimba juu

1. Walikombolewa waimba juu, wakisujudu mbele zake Bwana. Huzuni na taabu zake dunia Bwana amewaondolea zote.

Pambio:
Wanamwimbia Mwana Kondoo aliyekufa, sasa yu hai, ameyashinda mauti.

 

2. Wanashika vinubi mikononi wakiimba wimbo wa Mwana Kondoo na Musa mtumishi wake Mungu, wakifurahia kushinda kwake.

 

3. Wasiopenda kumsujudia, katika dunia hii ya sasa. Hawataonekana mbele zake, watateketea motoni kweli.

 

4. Mda unaobaki ni mfupi, tujitayarisheni ndugu sasa. Bwana ajapo tuwepo tayari, tutaimba naye kule mbinguni. 




308 Naona maajabu leo

1. Naona maajabu leo (yatoka) yatoka Bwana Mungu wetu (wa kweli) Katika maahadi yake,

(Ishara) Ishara zinaonekana.

(Naona) naona majabu kubwa,

(Napenda) napenda kushukuru Bwana.

(Kwa nini) kwa kuwa anapenda mimi,

(Ishara) ishara kubwa kutoka Mungu.

 

2. Kati dunia yote hii (ni mambo) ni mambo mengi ya ajabu (ni Yesu) ni Yesu anapita wote (kufanya) kufanya maajabu mengi. 3.Ni kama tetemeko kubwa (itembe’ ) itembeayo ndani yangu (nikiku’) ninikumbuka Yesu Kristo (ya kuwa) angali anipenda mimi.

 

4. Viziwi na viwete vyote (na bubu), vipofu na wakoma wote (na wafu), na wafu walifufuliwa (kwa jina) kwa jina lake Yesu Kristo.

 

5. Mapendo yake Mungu kwangu (makubwa), yananibembeleza vema (upendo), upendo wake Yesu Kristo (ni dawa), ni dawa manukato kwangu.

(Sauti), sauti ya Mungu yasema:

(Ni huyu), ni huyu Mwanangu mpendwa

(Napenda), napendezwa na kazi yake,

(Sikia), sikieni maneno yake.

TAMBI Eae Munaongo, 1949




309 Mungu akasema iwe nuru, ikawa nuru

1. Mungu akasema iwe nuru, ikawa nuru, Mungu akaona nuru yakwamba ni njema. Mungu akatenga nuru na giza, Mungu akaiita nuru mchana, na giza akaliita usiku. Ikawa asubuhi, ikawa jioni, siku moja.

 

2. Mungu akasema na liwe anga, katikati ya maji. Likayatenge maji na maji, Mungu akalifanya anga. Akayatenga yale maji yaliyo juu ya anga, na yale maji yaliyo chini ya anga. Ikawa hivyo. Mungu akaliita lile anga mbingu. Ikawa jioni, ikawa asubuhi, siku ya pili.

 

3. Mungu akasema, maji yaliyo chini ya mbingu, na yakusanyike mahali pamoja, ili pakavu paonekane, ikawa hivyo. Mungu akapaita pale pakavu nchi. Na makusanyiko ya maji akayaita bahari. Mungu akaona ya kuwa ni vyema kuwa ni vyema.

Mwanzo 1: 3-10
TAMBI Eae Munaongo, 1960




310 Ukitafuta wokovu, dhambi zivutwe.

1. Ukitafuta wokovu, dhambi zivutwe. Twakuletea habari, Yesu anakuita.

Pambio:
Yesu Mwokozi akuita, akuita, akuita Yesu Mwokozi akuita, akuita wewe leo.

 

2.Ukipotea dhambini mbali na Mungu wako, Yesu aliyekufia anakuita leo.

 

3. Wewe uliyesikia mwito wa Yesu leo, usichelewe kufika, wakati wako leo.

 

4. Wengine walisikia, bali walipotea. Hawakujuwa wakati wao wakuokolewa.

Missionnary, 1956




311 Mara kwa mara Yesu aita, umwitikie sasa.

1. Mara kwa mara Yesu aita, umwitikie sasa. Yawezekana ni mara mwisho, anakuita sasa.

Pambio:
Wewe uliye dhambini, Yesu akutafuta. Akusamehe makosa, usichelewe ndugu.

 

2. Machangamko ya kidunia hayatakupata (sic) raha. Na mapendezo ya wenye dhambi yakudanganya sasa.

 

3.Giza ya kufa huja upesi, siku usipojua. Rafiki yangu usichelewe, kumpokea Yesu.

 

4. Roho ikiwa nzito na dhambi, Yesu anakujua. Akupokea vile ulivyo, tena utaokoka.

 

5. Mwito wa Mungu unakujia, mara kwa mara ndugu. Ukikataa kumpokea, utapotea kweli.

Missionnary, 1954




312 Zaburi 117:1-2

1. Zaburi 117:1-2. Enyi mataifa yote, msifuni Bwana, enyi watu wote mhimidi. Maana fadhili zake, kwetu sisi ni kuu, na uaminifu wa Bwana ni wa milele.

Pambio:
Zaburi 118: 1-7,2. Mshukuruni Bwana, kwa kuwa ni mwema. Kwa kuwa fadhili zake ni za milele. Israeli na aseme sasa, ya kwamba fadhili zake, ya kwamba fadhili zake ni za milele.

 

2. Mlango wa Haruni na waseme sasa, ya kwamba fadhili zake ni za milele. Wamchao Bwana na waseme sasa, ya kwamba fadhili zake ni za milele.

 

3. Katika shida yangu nalimwita Bwana. Bwana yuko upande wangu, sitaogopa; mwanadamu atanitenda nini? Bwana yuko upande wangu, msaidizi wangu, msaidizi wangu.

TAMBI Eae Munaongo, 1958




313 Kumbe wakati wapita mbio, ni sawa jana mlipofika,

1. Kumbe wakati wapita mbio, ni sawa jana mlipofika, mlitumika pamoja nasi, na sisi wote tulifurahi.

 

2. Na kazi yenu tuliipenda, hamkuchoka kutufurahisha. Taabu yenu haiko bure, ni Bwana Yesu atawalipa.

 

3. Mnaporudi mlikotoka twaomba Mungu mrudi tena. Kutumika pamoja nasi, kazi ni nyingi zinazowangoja.

 

4. Machozi mengi yalengalenga kwa macho yetu mnapotuacha, ni siku gani tutaonana. Mwenyezi Mungu ndiye ajua.

 

5. Salamu sana kwa nchi yenu, kwa makanisa na wakristo, sema Mwokozi ni Yesu peke, aliyekwisha kutusamehe.

 

6. Pasha habari ya ile hati ya mashitaki imetundikwa na imekazwa kwa nguvu sana, msalabani ifedheheke.

 

7.Na ile hati ya adui, ni Bwana Yesu ameifuta, hakuna tena hukumu kwetu tunaokaa ndani ya Yesu.

TAMBI Munaongo, 1955




314 Kuomba ni agizo jema mno, kupata ni ahadi tamu kweli

1. Kuomba ni agizo jema mno, kupata ni ahadi tamu kweli. Likiwa nene nguvu na matata; tazama afungaye kwa upendo.

Pambio:
Sifa kwa Mungu Baba wetu, Anawaunga wawili leo, Alicho unganisha Mungu Mwana adamu asitenganishe.

 

2. Tuombe kwa agizo la Mwokozi, tuliokuwa wenye kupotea, lakini sasa tunaunganishwa kwa jina lake Bwana Yesu Kristo.

 

3.Uwe rafiki yake Bwana Yesu, msiharibu pendo kwa maneno, mkiheshimu Mungu kati yote, amani ya Yesu ‘takuwa nanyi.

 

4. Mungu aliumba mme na mke na ikingali hivyo hata leo, na ninyi ndugu mnaunganishwa, katika jina lake Bwana Yesu.

 

5. Salamu hii toka sisi wote, neno la Mungu la kuwafariji. Wakolosai kwa sura ya tatu haya ya kumi na nane inatosha.

TAMBI Eae Munaongo, 1943




315 Baba Mungu akifunga, hata moja tafungua

1. Baba Mungu akifunga, hata moja tafungua. Na kama akifungua, wakufunga anakosa. Siku utatufungua tutaruka kama njiwa, Eh Mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyake Mungu.

 

2. Sisi watumishi wako, umetuachia kazi. Ili tuifanye kwa bidii na tungoje kuja kwako, watumishi wako Bwana. Tunaomba utulinde, Eh Mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyake Mungu.

 

3. Mara nyingi tunaona uchokozi wa dunia, kutupima roho zetu, kwa kutesa mwili wetu. Haleluya tutasifu Mkombozi wetu Yesu, eh Mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyake Mungu.

TAMBI Eae Munaongo, 1952




316 Nyota kubwa inang’aa, inang’aa nguvu sana,

1. Nyota kubwa inang’aa, inang’aa nguvu sana, ahadi ya zamani. Iling’aa tangu mbele manabii wali’ona, ilingoja wakati. :/: Iling’aa, nyota kubwa yang’aa. :/:

 

2. Manabii waliona nyota ile iling’aa ilikuwa kwa mbali. Na Bwana aliona nyota kutoka Yakobo kwa maono rohoni. :/: Iling’aa, nyota toka Yakobo. :/:

 

3. Mashauri ya mbinguni yalipokuwa tayari Mwokozi alifika. Nyota yake itang’aa kwa milele na milele, haizimike kamwe. :/: Itang’aa, itang’aa milele. :/:

 

4. Iling’aa, iling’aa, iling’aa, iling’aa, ilikuwa kwa mbali. Ni majusi walipata kuiona mashariki nyota ya Bwana Yesu. :/: Iling’aa, iliangaza wazi. :/:

 

5. Ni Isaya anasema kama mwana tumepewa, Mwokozi azaliwa. Anaitwa Wa ajabu na Mkuu wa amani, watu wake furahi. :/: Wa ajabu, Wa ajabu Masiya. :/:

 

6. Mashariki, Magaribi, Kaskazini na Kusini inaangaza pote. Watu wote wameisha kusikia Neno lake linaangaza wote. :/: Wa ajabu, Wa ajabu Masiya. :/:

 

TAMBI Eae Munaongo, 1949




317 Sisi tuliokoka na tunashangilia

1. Sisi tuliokoka na tunashangilia, twapita unlimwengu na tuna amani.

 

2. Mwapenda vya dunia mbona hamvishibe, hata wababu zenu hawakuviweza.

 

3.Dunia itaisha na vyote vilivyomo. Nyumba na mashamba, akili na pombe.

 

4. Vinavyowadanganya havitawaokoa, vitakuwa majivu, arudipo Bwana.

 

5. Na wenye roho ngumu, tuwafanyie nini? Mbona tunawaonya na mnakataa?

 

6. Hatuna la kufanya, tutahamia mbingu. Tunasikitika ju’ ya wenye dhambi.

 

7. Tutakwenda mbinguni, kuona wateule, vijana ‘takatifu waliotakaswa.

 

8. Tutashirikiana na makabila tena, ila waliotubu na kuoshwa na Yesu.

 

Wimbo wa kirundi
TAMBI Eae Munaongo, 1952




318 Nimeliona pendo kubwa mno

1. Nimeliona pendo kubwa mno, na pendo hilo nalifurahia. Na jina lake mwenye kunipenda, Ni Mungu Baba tena Yesu Mwana. :/: Upendo wako nausifu sana, ewe Mungu nawe Yesu Kristo. :/:

 

2. Mimi mtoto mdogo mbele yako, nakuhitaji unisaidie. Kwa kila kazi na kwa hali zote, kwa majaribu katika dunia. :/: Usiniache mimi peke yangu, uwe nami kwa safari yangu. :/:

 

3.Nikikuomba uje kwangu Yesu, ukija tena ninaona hofu. Utanishika mimi mwanadamu, sitendi vema mimi mwenye shaka. :/: Nilipendalo silitendi tena, ninafanya nisilolipenda. :/:

 

4.Nilipokuwa mtoto mchanga, na niliwaza mambo ya utoto. Na kwa wakati wakuwa mzima, nilibadili mambo ya utoto. :/: Matumaini na imani yangu, inakwamilishwa kwa injili. :/:

 

5.Nimeliona pendo la Mwokozi, aliyenikomboa kati damu. Na damu hiyo si damu ya nyama, ni damu yake Bwana Yesu Kristo. :/: Ee! Mwenye haki kwa wasio haki, umetoa maisha na pendo.:/:

TAMBI Eae Munaongo, 1942