Digg StumbleUpon LinkedIn YouTube Flickr Facebook Twitter RSS Reset

328 Bwana Yesu ‘tuongoze, wende mbele yetu

image_pdfsauvegarder en PDF-Saveimage_printImprimer-Print

1. Bwana Yesu ‘tuongoze, wende mbele yetu. Sisi tuwe nyuma yako, tufike Sayuni. Sisi peke hatuwezi kuongoza njia yetu. Ulisema peke yako, wewe ndiwe njia.

 

2. Huku chini duniani tunahangaishwa. Vinavyotuhangaisha vitabaki huku. Bwana Yesu tunachoka, tuwezeshe safarini. Kwa kungoja baragumu tushushie Roho.

 

3. Mambo mengi yanafichwa kwa kukosa moto. Watu wengi wanacheza na maovu yao. Wanadhani huwaoni, mwovu anawadanganya. Tuma uamsho, Bwana, urudishe wengi.

 

4. Twakwambia leo, ndugu, usidanganyike. Bwana Yesu anajua njia zako zote. Hata ikiwa usiku kwake kuna nuru wazi. Acha njia zile ndugu, saa zingaliko.

 

5.Usidhani hakuoni, anavumilia. Anangoja siku ile atimize yote. Una heri leo, ndugu, kwani tunakukumbusha. Fika leo kwa Mwokozi, saa zinapita.

 

6. Anabisha mlangoni, umfungulie, anataka aingie kuokoa wewe. Mbona humfungulie? Anakuhitaji wewe. Ne’ma kwako itakwisha, utahukumiwa.

 

7. Una heri, ndugu, wewe uliye hokoka, Bwana Yesu akirudi, tutashangilia. Tutamfanana Yesu, na kurithi mji ule, wa milele na milele, mji wa heri…

 

MUBIKWA Onesimo, 1964

No comments yet.

Leave a Comment