Digg StumbleUpon LinkedIn YouTube Flickr Facebook Twitter RSS Reset

322 Nashika njia ya kwenda mbingu

image_pdfsauvegarder en PDF-Saveimage_printImprimer-Print

1. Nashika njia ya kwenda mbingu, mimi msafiri duniani, naishi kwa taabu na mateso mengi. Bali nakaza mwendo nifike mbingu.

 

2. Ijapo shida zanizunguuka, mimi msafiri njia, nashika njia nifike mbingu; nitarithi pamoja na Yesu, nitarithi pamoja na Yesu. :/:

 

3. Wenzangu wote wananigombeza na marafiki wananicheka. Nasumbuliwa hata na wanangu, natazama Yesu rafiki Mwema.

 

4. Ninachofanya maishani mwangu, nimpendeze Mungu aliye Mwema. Nijapoteswa, ninatumaini kuingia mbingu, ni nchi ya raha.

 

MUSAFIRI Chidunga Chigangu, 1993

No comments yet.

Leave a Comment