Digg StumbleUpon LinkedIn YouTube Flickr Facebook Twitter RSS Reset

319 Nafurahia wokovu niliopata kwa Yesu

image_pdfsauvegarder en PDF-Saveimage_printImprimer-Print

1. Nafurahia wokovu niliopata kwa Yesu, nitasifu Mungu wangu daima huko mbinguni. Wokovu niliopewa, na unanirusha juu, kw’ajili ya shangwe kubwa, inayoimba rohoni.

 

2. Silinganishe wokovu wangu na kitu kingine. Kwani vyote vinakosa, bei ya wokovu wangu. Mwokozi alinifia, alinilipia damu, nayo ni ya bei ghali, safi ya Mwana wa Mungu.

 

3. Ninaupenda wokovu, wanitosha kwa matata, kwani Bwana wa wokovu, hakufuata makelele. Aliwaponya wagonjwa, na alifufua wafu, akahubiri injili, alituonyesha njia.

 

4. Ninakusifu Mwokozi, kwani umeniokoa, umenitosha kwa giza, na sasa niko nuruni. Mwenye upendo ni wewe, neema yake ni kubwa, ulinitosha kabisa, katitka pori na giza.

 

TAMBI, Ntoto 1955

No comments yet.

Leave a Comment