Digg StumbleUpon LinkedIn YouTube Flickr Facebook Twitter RSS Reset

276. MATENDO ya Mungu yapita fahamu

image_pdfsauvegarder en PDF-Saveimage_printImprimer-Print

276

1.  Matendo ya Mungu yapita ‘fahamu, ni nani ayaona wazi? Lakini najua mapito ya Mungu kwa mimi yafaa halisi.

 

2.Njiani sijui maana ya yote, lakini nitayafaamu. Kwa nini kuzisumbukia kwa bure taabu na shida za mda?

 

3. E’ Bwana, unayo magari maelfu, na lenye linalonifaa, u’lichagulie mwenyewe, Bwanangu, nifike salama mbinguni!

 

4.Na kama Elia upesi kabisa nitakavyoacha dunia, uchungu na shida za huku ‘takwisha, milele nitashangilia.

 

5. Tutamsujudu Mwokozi daima, kuimba maelfu pamoja: E’ Mungu, u haki na mwenye neema katika shauri na tendo.

 

6.Halafu nangoja kwa uvumilivu kujua maana kwa wazi. Na matumaini ni yenye uzima: Urithi ninao mbinguni.

 

Emil Gustavsson, 1886

4 Responses to “276. MATENDO ya Mungu yapita fahamu”

 1. Daniel RWIMO
  08/01/2016 at 7:58 am #

  MUNGU Aliye mbinguni astahili kupewa sifa. Bwana Yesu awabariki sana dada.

 2. 20/01/2016 at 3:27 pm #

  Tunashukuru sana, Mungu akubariki pia ndugu Rwimo

 3. Rose
  16/05/2016 at 9:43 pm #

  Mungu awabarikie naeza ku pata book za nyimbo wapi?

 4. Espoir BONDO
  05/01/2017 at 3:46 am #

  Que Le Bon Dieu vous Bénisses mes chère Sœurs.

Leave a Comment