Digg StumbleUpon LinkedIn YouTube Flickr Facebook Twitter RSS Reset

165 NITAZAMAPO kwa imani

image_pdfsauvegarder en PDF-Saveimage_printImprimer-Print

165

1. Nitazamapo kwa imani Mwokozi wangu, nafurahi, naona utajiri wake anao Mungu, Baba yangu. Haleluya! Furaha kubwa, aniongoza siku zote! Nikiuona udhaifu, anichukuwa mikononi.

 

2. Sitasumbuka mimi tena, furaha inanijaliza; Na kwa upendo na rehema anisikia, nikiomba. Haleluya! Ananitunza, Ninastarehe kwa salama. Na ukitaka raha yake, mfungulie moyo wako!

 

3.┬áNilipokaa kati’ dhambi Nikaliona sikitiko, Lakini shaka na hukumu Zimeondoka kwangu sasa. Haleluya! Anipa nguvu Yakuyashinda majaribu. Rohoni mwangu nina raha, Nalindwa nayo siku zote.

 

4. Dhihaka na mateso yote si kitu kwangu kwa sababu nafarijiwa na Mwokozi, nakumbatiwa na babangu. Haleluya! Mwokozi wangu ananitunza kwa neema. Nikiwa na ‘dhaifu tena, natiwa nguvu kwa imani.

Samuel Gustavsson, 1930

No comments yet.

Leave a Comment