Digg StumbleUpon LinkedIn YouTube Flickr Facebook Twitter RSS Reset

140 UKICHUKULIWA na mashaka yako

image_pdfsauvegarder en PDF-Saveimage_printImprimer-Print

1. Ukichukuliwa na mashaka yako na kuona hufu kwamba utakwama, uhesabu mibaraka yake Mungu, na utashangaa kwa rehema yake.

Pambio:
Uhesabu mibaraka yote Mungu aliyoyakubariki! Ukumbuke mambo yote pia, na utashangaa kwa rehema yake!

 

2. Na ukiudhiwa na huzuni nyingi, ukiona msalaba ni mzito, uhesabu mibaraka kuchwa pia, na kwa moyo wote utasifu Mungu.

 

3. Wengi watamani mali ya dunia; utajiri wako ni Mwenyezi Mungu. Uhesabu mibaraka na kumbuka: Mali haiwezi kufungua mbingu.

 

4. Na katika mambo yote huku chini ukumbuke pendo kubwa la Mwokozi! Na ujumlishe mibaraka yote, tena mwisho atakuchukua kwake!

Johnson Oatman Jr
When upon life’s billows, R.S. 5

One Response to “140 UKICHUKULIWA na mashaka yako”

  1. 21/01/2017 at 6:58 am #

    Hawa wa dada wameimba kwa sauti inayo stahili,ndivyo uimbwavyo wimbo huo

Leave a Comment