133 UFURAHI moyo wangu

1. Ufurahi, moyo wangu, heri nyingi umepata!
:/: Sikitiko limekwisha, Yesu ni wangu nami wake. :/:

 

2. Ameponya roho yangu, yeye ni mponyaji mwema;
:/: Na kwa Roho ‘takatifu anabatiza watu wake. :/:

 

3.Jina langu ni mbinguni, Yesu ameliandika.
:/: Mimi mali ya Mwokozi hata milele na milele.:/:

 

4.Na moyoni mwangu sasa ninaimba: Mungu, Baba!
:/:Ni furaha kubwa sana, nina rafiki kila saa. :/:

 

5.Nimeondolewa dhambi, nisitende ovu tena!
:/: Kwani Yesu aokoa kila wakati na dakita. :/:

 

6.Nyimbo za kusifu Mungu zinajaa mbingu zote.
:/: Moyo wangu unajibu: Amina. Mungu asifiwe» :/:

Emil Gustavsson, 1887