119 TUIMBIE msalaba wa Mwokozi

119

1. Tuimbie msalaba wa Mwokozi, damu yake inatusafisha sana! Tunaweza kuwa huru, kwani Yesu alikufa ili ku’ondoa dhambi.

Pambio:
Haleluya, anipenda! Haleluya nafurahi! Haleluya, siku moja nitamwona Yesu!

 

2. Twafurahi kwa neema yake kubwa, alikuja ili tuwe na uzima. Kama njia ni nyembamba duniani, Yesu atatupa nguvu na ‘hodari.

 

3. Tuuimbe moto ule ‘takatifu uli’tupwa na Mwokozi duniani! Tuvipige vita vilivyo vizuri, nasi tutapewa taji ya uzima!