Digg StumbleUpon LinkedIn YouTube Flickr Facebook Twitter RSS Reset

111 E’YESU sitasahau uchungu wako ‘kubwa

image_pdfsauvegarder en PDF-Saveimage_printImprimer-Print

111

1. E’ Yesu, sitausahau uchungu wako kubwa, ulipoteswa Gethsemane usiku peke yako.

Pambio:
Mateso uliyoyaona, uchungu na machozi, Usiku ule Gethsemane, Siyasahau kamwe.

 

2.Naona wewe Gethsemane, ulivyoteswa huko kwa ‘jili ya makosa yangu, na kuitoa damu.

 

3.Huzuni nyingi uliona katika teso lako ulipoachwa peke yako na wanafunzi wako.

 

4.Na ukiona roho yangu haina pendo kwako, uniongoze Gethsemane, nione teso lako!

Edward P. Hammond
Tune: O Lord, remember me

No comments yet.

Leave a Comment